AHOUA NA KIBU WANABALAA HAO WAISAMBARATISHA DODOMA JIJI

 Klabu ya Simba imeendelea kufanya vyema msimu  huu wa Ligi kuu ya NBC baada ya kuisambaratisha Dodoma jiji kwa mabao 6-0. Ushindi huo umewafanya simba wasogee kwa ukaribu nafasi ya kwanza kwa tofauti  ya alama 1 dhidi ya Yanga.


Tathmini ya Mchezo

Kocha Fadlu Davis aliingia na mfumo wa 4-3-3 ulioundwa na Ally Salim, David Kameta,Mohammed Hussein,Chamou,Abdurazak Hamza ,Yusuf Kagoma,Kibu Denis,Fabrice Ngoma,Steven Mukwala,Jean Charles Ahoua na Ellie Mpanzu.

Kikosi hicho kilionyesha makali yake kwa kupata bao la uongozi dakika ya 16 kupitia kwa Ellie Mpanzu, Jean charles Ahoua alipachika bao la pili dakika ya 21 na la tatu dakika ya 45,Simba walikwenda mapumziko wakiwa kifua mbele kwa mabao 3-0. Kipindi cha pili dakika ya 46 Steven Mukwala aliiandikia Simba bao la nne.

Kibu Denis aliipa Simba bao la tano dakika ya 55  na bao la sita dakika ya 

Jean Charles Ahoua ndiye kinara wa magoli msimu huu akifunga mabao 12 na kutengeneza pasi za mwisho 6 zilizozaa mabao.

Post a Comment

0 Comments