Kocha Suleiman Iddi Mmoroko ametangaza kikosi cha wachezaji 25 kitakachoingia kambini kujiandaa na mchezo wa kufuzu Kombe la Dunia dhidi ya Morocco zitakazofanyika mwaka 2026 nchini Marekani. kikosi hicho kimesheheni wachezaji kutoka ndani na nje ya nchi na mchezo huo utapigwa tarehe 26 jijini Casablanca Morocco.
Klabu ya Simba imetoa nyota watano ikifuatiwa na Yanga nyota wanne pamoja na Azam FC nyota wanne.Mbwana Ally Samatta amekosekana kwenye kikosi hicho kutokana na majeraha aliyoyapata akiwa mazoezini klabuni kwake na itamchukua wiki mbili hadi tatu kurejea kwenye utimamu.
Kwa upande wachezaji wengine kama Aishi Manula pamoja na Bakari Nondo Mwamnyeto kutokuitwa kwao inatokana na kutopata nafasi ya kuonyesha uwezo wao kwa klabu zao msimu huu.
Taifa Stars ipo kundi E ikiwa na alama 6 katika michezo 3 iliyocheza,UShindi dhidi ya Morocco utaipeleka kileleni mwa kundi linaloongozwa na Morroco wenye alama 9 katika michezo 3 waliyocheza.
Hiki hapa kikosi cha Taifa Stars


0 Comments