Simba wako tayari kuwakaribisha Dodoma jiji jioni ya leo kuelekea mchezo wa ligi kuu ya NBC utakaopigwa dimba la KMC Complex majira ya saa 10 jioni. Kwa mujibu wa taarifa rasmi iliyotolewa na msemaji wa timu hiyo Bw.Ahmed Ally amenukuliwa akisema.Wachezaji wote wako vizuri lakini watamkosa Shomari Kapombe mwenye kadi tatu za njano.
Simba wanapaswa kushinda mchezo huo ili kuendeleza mbio za ubingwa wa ligi kuu. Wapo nafasi ya pili wakiwa na alama 54 wakizipata katika michezo 21 . Mpinzani wake Yanga yupo nafasi ya kwanza akiwa na alama 58 alizozipata kwenye michezo 22, Ushindi huo utawafanya Simba kufikisha alama 57 na kubakiza alama 1 pekee kuelekea kileleni.
Mara baada ya mchezo huo wachezaji watano akiwemo Ally Salim Katoro,Kibu Denis,Shomari Kapombe,Muhammed Hussein na Abdulrazack Hamza Mohammed watajiunga na kambi ya kikosi cha timu ya taifa Taifa Stars kuelekea Morocco kwenye mchezo wa kufuzu kombe la dunia tarehe 26 Machi.

0 Comments