TAIFA STARS: WALETENI HAO WAMOROCCO TUWAONYESHE UWEZO WETU

 Kikosi cha timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars leo usiku kitavaana na Morocco mchezo wa mzunguko wa tano wa kundi E kuwania kufuzu Kombe la Dunia mwaka 2026 nchini Marekani.Stars wako nafasi ya 3 wakiwa na alama 6 katika michezo waliyocheza. Kundi E linaongowa na Morocco wenye alama 12 wakifuatiwa na Niger wenye alama 6.



Ushindi wa Taifa Stars utaipeleka timu katika nafasi ya pili na hilo litategemea endapo Niger watapoteza au kutoa sare na Bonaire.

Tathmini ya Mchezo 

Taarifa kutoka Morocco zinasema wachezaji wote wako timamu kwa ajili ya mchezo huo utakaopigwa saa 6:30 usiku kwa saa za Africa Mashariki.Kikosi cha Stars kimesheheni nyota mbalimbali wanaocheza ligi kuu ya NBC na ligi mbalimbali Duniani.

Kocha Hemed Mmoroco anatambua thamani ya mchezo huo hivyo tutegemee umakini wa kimchezo kwanzia upangaji wa kikosi,,Mbinu za kiuchezaji na malengo ya mchezaji mmoja mmoja ndani ya kiwanja. 

Msuva,Kibu Denis,Clement Mzize na Feisal Salum wanaweza kutumika kuiangamiza safu ya ulinzi ya Morocco.Kikosi kilichopo Morocco kimesheheni nyota wenye uzoefu na mechi kubwa hivyo wachezaji kama Hakim Ziyech,Mazraoui,Brahim Diaz na Achraf Akim wanaweza kuthibitiwa na magwiji wetu.

Rekodi ya Stars dhidi ya Morocco

Taifa Stars imekutana na Morocco katika michezo 6.Morocco imeshinda michezo 5 na kufunga mabao 12 wakati Stars imeshinda mchezo 1 na kufunga jumla ya mabao 5.Mara ya mwisho timu hizo kukutana ni 2024 mchezo uliomalizika kwa Morocco kushinda kwa mabao 3-0.

Tanzania iliifunga Morocco mwaka 2013 na tangu hapo tumekuwa wateja wa Morocco kwani walitufunga kwenye michezo ya kufuzu Afcon na Kombe la dunia.Usiku huu wa leo utumike kuvunja mwiko wa kufungwa na timu hiyo

Post a Comment

0 Comments