Tottenham imeendelea kufanya vibaya msimu huu baada ya kuruhusu kipigo cha mabao 2-0 dhidi ya Fulham.Huu ni mchezo wa tatu mfululizo kwa klabu hiyo kupoteza alama na kuwafanya kusalia nafasi ya 13 katika mechi 29 walizocheza mpaka sasa huku wakijikusanyia alama 34 pekee.
Spurs wamekuwa na msimu mbaya zaidi kwa kipindi cha miaka10 iliyopita.Klabu hiyo imekuwa bora katika safu ya Ushambuliaji wakifunga mabao 55 lakini eneo la Ulinzi limekuwa tatizo kwani limeruhusu mabao 43.Timu hiyo imepoteza michezo 15 ikipata sare 4 na kushinda michezo 10 pekee.
Tottenham wanaonekana kuwa na nyakati mbaya EPL ikiwa ni moja ya timu 9 zilizofungwa mabao zaidi ya 40. Nafasi waliyokaa kwa sasa si rasmi kwani Manchester United walio nafasi ya 15 wakiwa na alama 33 na wanamchezo dhidi ya Leicester City kama watashinda basi watafikisha alama 37 na kupanda mpaka nafasi ya 13 wakati Spurs wakiporomoka.
Mategemeo ya kurejesha ubora wao EPL
Mwezi April Tottenham atakuwa na kibarua kigumu dhidi ya Chelsea,Liverpool na Nottingham . Mechi hizi ni ngumu sana kwake kutokana na kila timu kuwa na malengo yake.Liverpool wanataka washinde mechi hiyo ili kujiwekea mazingira mazuri ya kutwaa ubingwa,Chelsea na Nottingham wanataka kusalia nafasi nne za juu hivyo matokeo chanya katika mchezo huo yatarudisha matumaini.
Mwezi Mei watakutana na Crystal Palace,Aston Villa,Brighton timu ambazo zipo juu yake kwenye msimamo wa ligi na Westham ambaye wamelingana alama kwenye msimamo wa ligi.
Kama Tottenham watabadilika wanaweza kufanya jambo,Mechi 9 zilizombele yao sawa na alama 27 zinaweza kuzaa mwanzo mpya kwao. Hawawezi kuwekwa kundi moja la timu inayowania ubingwa bali kundi la timu inayoweza kushiriki michuano ya Europa League au Conference league.
Wataweza kufanya maajabu kombe la Europa
Tottenham na Manchester United zimefanikiwa kutinga robo fainali ya kombe la Europa hatua ya robo fainali, katika hatua hizo watakutana na Frankfurt ya ujerumani,Mchezo wa kwanza utapigwa April 10 jijini Uingereza na mchezo wa marudiano utapigwa April 17 kama watavuka hatua hizo watatinga nusu fainali na yawezekana kufika fainali na hatimaye kutwaa ubingwa wa Europa.

0 Comments