Ligi kuu Uingereza inaendelea tena jioni ya leo kwa mchezo mwingine mgumu unaowakutanisha magwiji wa London Arsenal wakiwa dimba la nyumbani Emirates dhidi ya Chelsea. Mchezo huu ni muhimu kwa pande zote kulingana na nafasi walizopo kwenye msimamo wa ligi.
Arsenal mwenyeji yupo nafasi ya pili akiwa na alama 55 ,Arsenal ametofautiana na Liverpool kwa alama 15 ushindi wa mchezo huo utapunguza gepu la alama mpaka 13 na kurejesha matumaini ya kuwania kutwaa ubingwa wa EPL kwa mara ya 14 katika historia.
Chelsea wako katika nafasi ya nne wakiwa na alama 49 ,Ushindi wa mchezo huo utawafanya wafikishe alama 52 na kusalia eneo hilo na kujiweka karibu kupanda nafasi ya tatu inayoshikiliwa na Nottingham Forest wenye alama 54. Mchezo huu ni muhimu kwa Mallersca na kikosi chake kwani wameofautiana kwa alama moja pekee na Manchester City aliye nafasi ya 5 akiwa na alama 48 katika michezo 29.
Tathmini ya Mchezo
Arsenal wamekuwa na wakati mbaya katika mechi zake 5 zilizopita wamepata ushindi mechi mbili kisha wakafungwa na kupata sare katika michezo miwili mfululizo ukiwemo dhidi ya Manchester United uliopigwa Old Trafford.
Arsenal wamebakiwa na karata mbili tu za makombe mawili kati ya manne waliyokuwa wakiyawania mwanzoni mwa msimu. UEFA wamepangwa na Real Madrid robo fainali na ligi kuu dhidi ya Liverpool walio kileleni.Imani ya Mkufunzi Mikel Arteta inamfanya azidi kuweka malengo makubwa katika mchezo wa leo.
Arteta ameanza na Raya,Jullen Timber,William Saliba,Gabriel ,Lewis,Odeegard,Partey,Rice,Martinelli,Trossard na Merino akitumia mfumo wa 4-3-3
Chelsea wamerejea kwenye kiwango baada ya kupoteza michezo miwili mfululizo kisha kurejea kwa kasi na kushinda michezo miwili mfululizo ukiwemo mchezo wa mwisho dhidi ya Leicester City umerudisha morali ya upambanaji kwa vijana wa Mallesrca.
Enzo Maresca ameanza na mfumo wa 4-2-3-1 Unaoundwa na Sanchez,Fofana,Badiashile,Colwill,Cucurela,James,Caicedo,Sanchez,Fernandez,Nkuku na Pedro Neto.
Tutegemee mabadiliko makubwa ya kiuchezaji katika mchezo wa leo kulingana na msimamo wa lig.

0 Comments