KANE,MBAPPE NA HALAAND WAGEUKA GUMZO ULAYA

 Mbio za ufungaji Bora msimu wa 2025/26 zimwendee kushika Kasi katika Ligi mbalimbali barani ulaya. Ushindani huu umewafanya Kylian Mbappe wa Real Madrid awe tishio La Liga akipachika mabao 11 katika Michezo 10 aliyocheza mpaka sasa.

Halaand amendelea kuwa tishio kwa Ligi kuu Uingereza baada ya kupachika mabao 11 katika mechi 9 alizoitumikia klabu Yake ya Manchester City. 

Harry Kane amekuwa mwiba makali Bundesliga akipachika mabao 12 katika mechi 8 alizocheza.

Mbali na kutikisa Ligi za nyumbani washambuliaji hao wameendelea kuwa gumzo kwenye michuano ya ligi ya mabingwa Ulaya. Halaand amefunga mabao 4 mpaka sasa akishika nafasi ya pili nyuma ya Mbappe mwenye mabao 5 Sawa na Hary Kane.

Ubora wa nyota hawa unaleta hisia mpya miongoni mwa mashabiki wa soka duniani wakihoji yupi ndiye mshambuliaji hatari zaidi  kwa SASA? Wanasema namba hazidanganyi na mwisho wa msimu tutazungumza mengi kuelekea kombe la dunia 2026 pale marekani .






Post a Comment

0 Comments