Taarifa hii imeripotiwa na mwandishi nguli wa habari za Michezo nchini Saleh Jembe
DP world ndio waendeshaji wa Bandari Kuu tatu kubwa za Dubai na United Arab Emirates.
Mwaka jana kwa udhamini wao nilipata nafasi ya kutembelea Bandari zao 3 za
Jebel Ali Port, Port Rashid, na Port Said.
Jebel Ali, ndio Bandari kubwa zaidi kwa Ukanda wa Mashariki ya Kati, hii ni Mpya na mimi na wenzangu tuliitembelea ya mwisho.
Kwa kuwa ndani ya Simba kwa muda mrefu kumekuwa na sakata la kwamba wanataka atoke mwekezaji wa sasa MO Dewji ili wachukue wao, mwisho niliona niwaulizie. Sababu niko hapa Cape Town, Afrika Kusini, ofisi yao kubwa zaidi Barani Afrika.
Mmoja viongozi wa DP World wanaosimamia uendeshaji wa Bandari hizo tatu za Dubai na Capetown Afrika Kusini, kaniambia hawawezi kuzungumzia jambo ambalo hawajahi kuwa na mpango nalo na AKASISITIZA hizi ni HADITHI WANAZOSOMA NITANDAONI.
"NI kweli tunashiriki michezo na hasa udhamini, hatuna mpango wa kumiliki klabu hata hapa kwetu. Sasa tuko kwenye gofu, kriketi na Formula 1," alisema.
"Katika soka labda udhamini baadaye sana... Kumiliki klabu si jambo letu sababu kazi yetu ni usafirishaji. Tulizungumza udhamini na kiongozi wao mkuu lakini mwisho hatukuwa na bajeti, sasa umiliki itawezekanaje," kilieleza chanzo changu cha uhakika.
Taarifa za kuwa DP World wanaitaka Simba kuimiliki au kuidhamini limekuwa likisambazwa lakini haijulikani Nani hasa mhusika Mkuu.
Baadhi inaelezwa ni wale wanaotaka kusababisha migongano kwa makusudi ndani ya klabu hiyo kwa maslahi yao binafsi.
Nikiripoti kutoka Cape Town, Afrika Kusini, mimi ni Saleh Ally Jembe...

0 Comments