WANANCHI WALIOPAGAWISHWA NA DIARRA WAMJIBU KWA VITENDO

 Golikipa namba Moja wa Klabu ya Yanga Djigui Diarra amewakonga wananchi kwnye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Js Kablye mchezo uliomalizika kwa Sare ya 0-0

Katika mchezo huo uliopigwa jijini Algiers nchini Algeria Diarra alionyesha kiwango cha hali ya juu kwa kuokoa michomo mikali kutoka kwa wapinzani wake. Huu ni mchezo wa pili mfululizo wa Ligi ya Mabingwa Africa kwa Golikipa huyo kuonyesha ubora wake kwa kutoruhusu bao ndani ya dakika 180 huku Yanga ikijikusanyia alama 4 na kushika nafasi ya pili kwenye msimamo wa kundi A nyuma ya Al Ahly.

Mashabiki wamuandalia Zawadi Nono

Kiwango kizuri alichokionyesha katika mchezo huo kimepelekea Mashabiki wa Yanga kuguswa na kuanzisha kampeni ya "kibegi cha maokoto" na kumkabidhi kiasi cha fedha pindi atakapowasili nchini mchana wa Leo majira ya Saa 7 

Mpaka tunaingia studio tayari kiasi cha shilingi milioni 2 kilikuwa kimekusanywa na muitikio wa wachangiaji umekuwa mkubwa.

Kocha Goncalez anastahili pongezi 

Kocha mkuu wa klabu ya Yanga Goncalez anastahili pongezi za Hali ya juu kwa namna Yanga ilivyocheza kwa kiwango cha hali ya juu katika Michezo yote miwili ya makundi na kuvuna alama 4. Kocha huyu amekabidhiwa timu hiyo hivi karibuni lakini amefanikiwa kupenyeza mbinu zake za kiufundi ambazo kwa sasa zinaleta matokeo chanya.

Katika mchezo dhidi ya Js Kablyie Kocha huyo aliwaanzisha Djigui Diarra , Israel Mwenda, Mohammed Hussein,Dickson Job na Ibra Bacca katika eneo la ulinzi. Mudathir Yahya,Duke Abuya ,Pacome zouzoua na Maxi nzengeli walipangwa eneo la kiungo ,Prince Dube na Ecua ndiyo walisimama  katika Safu ya ushambuliaji.

Kikosi hiki cha Yanga kilimiliki mpira na kucheza kwa ufanisi huku kikifanya mashambulizi ya kushtukiza Jambo lililowapa wakati mgumu zaidi Js Kablyie.




Post a Comment

0 Comments