Klabu ya Liverpool imeendelea kupitia wakati mgumu msimu huu baada ya kuruhusu kipigo cha mabao 3-0 dhidi ya Nottingham Forest . Hiki ni kipigo cha Sita kwa Liverpool katika mechi 12 za Ligi kuu walizocheza msimu huu.
Liverpool wameshinda mechi 6 pekee za Epl wakifunga mabao 18 na kuruhusu mabao 20 ikiwa ni rekodi mbaya zaidi kwa siku za karibuni na hii inamweka katika wakati mgumu kocha Arne Slot aliyerithi mikoba ya Jürgen Slot mwishoni mwa msimu wa 2024/25.
Sajili zashindwa kuzaa matunda
Hugo Ekitike,Jeremie Frimpong,Alexander Isak,Milos Kerkez,Giovanni Leoni,Armin Pecsi,Florian Wirtz,Freddie Woodman,will Wright na Giorgi Mamardashvii ni majina ya wachezaji waliosajiliwa msimu huu lakini mpaka sasa hawajaleta matokeo yaliyokusudiwa.
Zaidi ya kiasi cha Paundi milioni 446 zimetumika kuwasajili nyota hao na Alexander Isak ndiye aliyeweka rekodi ya kununuliwa kwa gharama kubwa zaidi ya Paundi milioni 125 akifuatiwa na Wirtz Paundi milioni 116.5 na Hugo Ekitike Paundi milioni 79.
Kocha Arne Slot anahitaji muda zaidi kujenga timu yenye Ushindani akiwatumia nyota hawa aliowasajili msimu huu.
Hali ya viwango vya Mohammed Salah na Alexander Isak
Msimu wa 2024/25 ulikuwa Bora zaidi kwa Salah baada ya kufunga mabao 29 katika Michezo 38 ya Ligi na kumfanya aibuke kinara WA ufungaji Bora na kuiwezesha Liverpool kutwaa ubingwa wa 20 wa EPL. Salah aliweka rekodi nyingine ya kutengeneza mabao 18 katika Michezo 38 na kwa Jumla alihusika Moja kwa Moja katika mabao 47 kwenye Michezo 38 na mafanikio hayo yalimwezesha kutwaa tuzo ya mchezaji Bora wa mwaka wa Uingereza PFA AWARDS
Alexander Isak alishika nafasi ya pili nyuma ya Salah katika mbio za ufungaji akiwa na mabao 23 katika Michezo 34 akiwa Newcastle United na aliiwezesha timu hiyo kutwaa ubingwa wa Efl cup.
Msimu wa 2025/26 NI mbaya zaidi kwa nyota hao kwani Mo Salah amefunga mabao 4 pekee katika Michezo 12 na Alexander Isak akifunga bao 1 pekee wote wakiwa tegemezi ndani ya Liverpool.
Kuna mategemeo ya kutetea ubingwa?
Arsenal wanaongoza msimamo wa Ligi wakiwa na alama 29 ,Liverpool wako nafasi ya 11 wakiwa na alama 18 Sawa na tofauti ya alama 11.
Ni mapema mno kuwatoa Liverpool katika mbio za ubingwa kwa sababu bado kuna Michezo 26 na wanaweza kurejea katika ubora wao wakati wowote na hii ni EPL Ligi yenye Ushindani wa kweli

0 Comments