ARSENAL YAANZA VIBAYA DISEMBA

 Klabu ya Arsenal imekubali kipigo cha mabao 2-1 kutoka kwa Aston Villa. Katika mchezo huo wenyeji wa mchezo Aston villa walikuwa wa kwanza kupata bao la uongozi dakika ya 36 kupitia kwa beki Matty Cash  na kipindi cha kwanza kumalizika wenyeji wakiwa kifua mbele.

Dakika ya 52 Kiungo Leandro Trossard alisawazisha bao hilo lakini Emiliano Buendia alirejesha shangwe kwa Astonvilla akipachika bao la ushindi dakika ya 90+5 na kuwafanya Arsenal kupoteza mchezo wa pili katika mechi 15 walizocheza mpaka sasa.

Arsenal wanaendelea kuongoza ligi kuu Uingereza wakiwa na alama 33 wakipata ushindi kwenye michezo 10 sare 3 na kupoteza 2.Nafasi ya pili inashikiliwa na Aston Villa wenye alama 30 wakicheza michezo 15 ushindi mechi 9 kupoteza mechi 3 sare mechi 3.

Mwendelezo wa EPL wikiendi hii

EPL inaendelea wikiendi hii kwa mechi mbalimbali. Chelsea watakaribishwa na Bournemouth FC, Everton watakuwa nyumbani kuwakabili Nottingham forest, Manchester City watawakaribisha Sunderland ,Newcastle watakuwa nyumbani dhidi ya Burnley na Tottenham watawakaribisha Brentford  mechi zote zitaanza saa 12 jioni na mchezo wa kuvutia zaidi ni Leeds wakiikaribisha Liverpool mchezo utakaopigwa saa 2;30 usiku .

Post a Comment

0 Comments