Kapteni wa Manchester United ,Bruno Fernandez amesikitishwa na uongozi mbovu wa klabu kwa maamuzi mabaya wanayoyafanya yakiigharimu klabu hiyo. Nyota huyo mwenye miaka 31 ameitumikia United kwa Misimu na sasa amechoshwa na uwajibikaji mbaya wa viongozi.
Mwishoni mwa msimu uliopita klabu ya Manchester United ilipokea ofa ya Paundi milioni 80 kutoka Al Hilal klabu ya Saudi Arabia lakini nyota huyo pamoja na kocha wake Reuben Amorim waliikataa ofa hiyo na Bruno alinukuliwa akisema "bado anaipenda united".
Sare ya mabao 4-4 dhidi ya Bournemouth imemuibua tena nyota huyo na sasa amenukuliwa akisema
"Upande wa klabu NI kama hawanihitaji kwa sababu walisema kama nitaondoka haitakuwa mbaya kwao na hili liliniumiza kiasi"
"Mbali na kuumizwa ilinifanya nihuzunike kwa sababu Mimi NI mchezaji ninayekuwepo nyakati nzuri na mbaya na ninajitoa kwa asilimia 100 lakini inafika wakati pesa kwao ni muhimu kuliko chochote".
"Msimu uliopita nilipokea ofa kutoka klabu kubwa iliyotwaa makombe mengi lakini niliikataa ,kwa tulipofikia sasa hata kama klabu ya Saudi Arabia itanihitaji basi nitakwenda huko walau watoto wangu wakapate Kuota jua baada ya miaka 6 si kama hapa Manchester ambapo baridi na mvua vimetawala"
Bruno alijiunga na United mwaka 2019 na ameitumikia klabu hiyo katika Michezo 307 mpaka sasa na kama itapaswa kuuzwa basi thamani yake ni Paundi milioni 57.
Hizi NI takwimu za Bruno tangu alipojiunga na Manchester United
Mbali na sakata la Bruno Fernandez United inapitia changamoto kwa baadhi ya wachezaji akiwemo Kobbie Maino ambaye kwa sasa anakosa nafasi za kuonyesha uwezo wake na meneja wake ameanza taratibu za kumtafuta klabu nyingine. Wachezaji kama Mc Tomminay,Greenwood wameendelea kuonyesha uwezo mzuri huko walikopelekwa.


0 Comments