HII HAPA MIGOGORO MITANO INAYOITESA SIMBA

 Klabu ya Simba imejikuta ikikalia kuti kavi kwa kipindi cha hivi karibuni na kujikuta ikizalisha migogoro mipya kila Leo. Mashabiki ,viongozi na wachezaji wamejikuta wakikosa majibu kuhusu chanzo cha migogoro hiyo huku wachambuzi na wadau wa soka nchini wakichochea migogoro hiyo kwa kiasi kikubwa.


Amospoti imeingia site na kubaini mambo kadhaa yanayopelekea kutokea kwa migogoro hiyo. 

1. SIMBA YAANZA VIBAYA CAF CHAMPIONS LEAGUE 

Klabu ya Simba imeanza vibaya kampeni zake za Ligi ya Mabingwa ulaya baada ya kupoteza kwa mabao 2-1 dhidi ya Stade Mallein ugenini kisha kupoteza kwa bao 1-0 dhidi ya Petro de Luanda uwanja wa Benjamin mkapa. Matokeo hayo yameiweka Simba katika nafasi ya mwisho katika kundi A na matokeo hayo yalipelekea kocha wake mkuu kutimuliwa. Mashabiki walihoji je tatizo ni kocha ama uongozi mbovu ulioshindwa kufanya sajili za uhakika wakati wa dirisha kubwa. 

Wengi walihoji sababu hasa za kuondoa kwa Israel Mwenda na Mohammed Hussein ambao wamehamia Yanga na wanaupiga mwingi tena wapo kikosi cha Kwanza. Baadhi ya Mashabiki wamekuwa wakilaumu namna timu Olivyocheza na mtazamo wa benchi la ufundi. Jambo hili limekuwa likiwapa wakati mgumu Sana Mashabiki .

2. MKUTANO MKUU WAMALIZIKA BILA MUAFAKA

MKUTANO mkuu ulimalizika na kuacha maswali yaliyokosa majibu kwa Mashabiki wa Simba. Wengi walihoji,wakashauri na mwisho wakataka kujua mwelekeo mpya wa Simba hasa suala la mabadiliko ya kiuendeshaji. Mwenyekiti Muktadha Mangungu alimaliza mkutano huo bila kutoa majibu ya maswali hayo na kuibua sintofahamu miongoni mwa wanachama na ikapelekea kuwepo kwa fukuto la kutokuwa na Imani na mwenyekiti huyo pamoja na bodi nzima ya klabu ya Simba.

3.UDHAMINI WA DP WORLD WAIBUA JANGA

Wengi wanaamini Mohammed Dewji ndiye aliyeleta ugumu kwa DP world kuwekeza ndani ya Simba lakini mwekezaji huyo amekuwa akipinga uzushi unaonenezwa kuhusu suala hilo na alifafanua kwamba DP WORLD walikuja kudhamini ndani ya Simba na Si kuwekeza lakini walishindwana kutokana na DP world kutofikia kiasi cha fedha kilichokusudiwa ambapo nafasi Yake ilikwenda kwa Betway. 

Jambo hili bado ni kigugumizi na linaonekana kukosa ufafanuzi WA kueleweka miongoni mwa wadau wa Simba na kupelekea mgogoro uzidi kupamba Moto.

4.KUPOTEZA MCHEZO DHIDI YA AZAM FC

Mara baada ya Simba kupoteza dhidi ya Stallien na Petro de Luanda Simba walimtimua kocha mkuu na mikoba kukabidhiwa Kocha msaidizi Suleiman MATOLA na jukumu lake la Kwanza NI mchezo dhidi ya Mbeya City mchezo ambao Simba waliibuka na ushindi WA mabao 3-0 wakionyesha kandanda Safi . Mchezo wa pili dhidi ya Azam FC mchezo ambao Simba walipoteza kwa mabao 2-0 na hapo kukaibuka mgogoro mwingine. Kwanini kila siku MATOLA anabaki kama kocha msaidizi na kwanini kocha mkuu anapokuja asije na msaidizi wake? . Mashabiki wamekosa Imani na MATOLA na sasa wanataka kocha mkuu ajaye aje na msaidizi wake na MATOLA aondoke. Jina la Gamondi linatamkwa na inasemekana mara baada ya AFCON kocha huyo atatua msimbazi na hapo ndipo tutajua mbivu na mbichi kwa Matola.

5.KAULI YA HERSI WASABABISHA MPASUKO 

Wakati akifanya presentation kwenye mkutano wa  FIFA uliofanyika Doha hivi karibuni bwana HERSI Saidi ilitumia video za Mashabiki wa Simba kuonyesha Hali ilivyo kwa vilabu vyetu na akasema migogoro imechangia kuharibika kwa soka la Africa.

Mfano huu haukupokewa vyema na Mashabiki wa Simba na kupelekea kuibua vita ya maneno ndani ya klabu wengi wakiutuhumu uongozi wa Mangungu na namna ulivyoshindwa kuleta mabadiliko mpaka kutolewa mifano mibaya duniani. Kwa sasa sakata Hilo limepamba moto

Post a Comment

0 Comments