Zikiwa zimesalia siku 9 kufika siku ya Christmas, klabu ya Simba kwa kushirikia n na mzabuni wake wa Jezi Jayrutty wametoa ofa ya jezi zote original zinazozalishwa na kusambazwa na kampuni hiyo.
Kupitia mkutano na waandishi wa habari msemaji wa klabu hiyo Ahmed Ally ametangaza ofa ya jezi hizo kutoka bei ya shilingi 45,000 Hadi 12,000 kwa jezi za Ligi kuu ,Ligi ya Mabingwa pamoja na jezi za watoto na jezi hizo tayari zipo madukani.
Sambamba na hilo klabu hiyo kwa kushirikiana na kampuni ya Jayrutty wametangaza tovuti maalumu itakayowasaidia wadau kuchagua na kununua jezi pamoja na vifaa vingine vyenye chapa ya Simba kisha watazipata jezi zao kupitia shirika la posta ambalo lina ofisi nchi nzima.
Hizi NI nukuu ambazo semaji Ahmed Ally alinukuliwa akisema
“Tunachofanya Simba na JayRutty ni kwenda na kasi ya dunia. Tumeamua kufungua soko letu kwenye digital ili watu wapate jezi kwa urahisi. Tukienda na punguzo hili la jezi lakini pia tunarahisisha mtu kupata jezi yake.”
“Pamoja na kwamba tunatoa punguzo la msimu wa sikukuu lakini pia tunapambana na jezi fake. Kama Mwanasimba alikuwa ananunua jezi fake Tsh. 15,000 sasa jezi original ataipata kwa Tsh. 12,000. Uamuzi ni kwako Mwanasimba.”
“Bei hii ya punguzo inaanza leo Desemba 16, 2025 na itakwenda hadi Januari 30, 2026 hivyo tuna siku 45 za ofa hii. Na kuna watu wanakwenda nyumbani sikukuu, usikubali kwenda mikono mitupu, nunua jezi za Simba uende na zawadi.”
“Unaweza kupata jezi hii hata kwa kukopa. Mitandao yote ya simu wanakopesha wateja wao hivyo unaweza kukopa sasa na kupata jezi yako. Hii fursa hatupaswi kuichezea hata kidogo, huu ndio wakati wa kila Mwanasimba kununua jezi yake original.”"Namna ya kuipata jezi hii ya ofa itakuwa kwa njia ya mtandao, kwa watu wanaotumia smart off au kiswaswadu. Kuipata itakuwa kwenye website ya jayruttyshop.co.tz utanunua jezi yako na unaweza kuipata kwa kutumia mitandao ya simu."-

0 Comments