Klabu ya Manchester City imeendelea kufanya vyema Ligi kuu ya Uingereza baada ya kuibuka na ushindi mnono wa mabao 3-0 dhidi ya Sunderland.
City walianza kupata bao la uongozi kupitia kwa Ruben Dias dakika ya 31 ,bao la pili likiwekwa kimiani na Gvadiol dakika ya 35 na Phil Foden kupachika bao la tatu dakika ya 65. Ushindi huo unawafanya City kupanda mpaka nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi wakiwa na alama 31 katika Michezo 15 wakitofautiana kwa alama mbili na vinara wa Ligi Arsenal.
HALI MBAYA KWA ARNE SLOT
Liverpool imeendelea kupitia wakati mgumu kwa kila mpinzani wanayekabiliana naye. Sare ya mabao 3-3 waliyopata dhidi ya Leeds inamfanya kocha Arne Slot azidi kuwa kwenye hatua za kupoteza kibarua chake
MANCHESTER UNITED YAIWINDA TOP 4
Ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya Wolvs umewafanya Manchester United kufikisha alama 25 sawa na Chelsea walio nafasi ya Sita kwenye msimamo a ligi .Shukrani za kipekee zimwendee Bruno Ferrnandes aliyepachika mabao 2 na pasi ya usaidizi katika ushindi huo mnono. Kwa sasa United wako nafasi ya sita wakipishana kwa alama 8 na vinara wa ligi hiyo Arsenal.
.jpg)
0 Comments