DEMBELE AMBWAGA TENA LAMINE YAMAL

 Ousmane Dembele na Aitana Bonmati wametawazwa kuwa wachezaji bora zaidi duniani katika Tuzo Bora za Fifa, nyota hao walifanikiwa kutwaa tuzo za Ballon d’Or mapema mwaka huu. 


Dembele alisaidia sana PSG kutwaa taji lao la kwanza la Ligi ya Mabingwa katika historia mwezi wa Mei, akifunga mabao 35 katika michuano yote kuelekea kile ambacho ni ushindi mtakatifu wa klabu hiyo ya Ufaransa.

Tuzo ya kocha bora wa mwaka wa wanaume ni Luis Enrique akiiongoza PSG kutwaa makombe yote waliyoshiriki, golikipa bora wa mwaka ni Dounarruma kutoka Psg. 

Kikosi Bora cha mwaka kimeundwa na


Rais wa Fifa Gianni Infantino - aliyetoka katika hafla ya droo ya Kombe la Dunia mjini Washington na kukabidhi Tuzo ya kwanza ya Amani ya Fifa, kwa Donald Trump - ndiye mgeni Rasmi nchini Qatar kwa sherehe hizo.


Post a Comment

0 Comments