PICHA:YANGA YAWASILI DODOMA KIBABE

 Klabu ya Yanga imewasili salama  jijini Dodoma kwa ajili ya mchezo wa Ligi kuu NBC dhidi ya Coastal Union hapo Kesho Saa 11:00 jioni katika dimba la Jamhuri Dodoma. 

Yanga wapo nafasi ya 3 katika msimamo wa Ligi wakiwa na alama 13 katika Michezo 5 wakishinda mechi 4 na sare 1 huku wakifunga mabao 11 na kuruhusu mabao 1 pekee.

Kama wanapata ushindi katika mchezo huo watafikisha alama 16 na kupanda mpaka nafasi ya 2 inayokaliwa na Pamba jiji kwa sasa wenye alama 16 katika Michezo 9.

Coastal Union wako nafasi ya 10 wakiwa na alama 9 wakicheza Michezo 7 ,ushindi mechi 2 ,sare 3 na kufungwa 2 kama wakishinda dhidi ya Yanga basi watapaa mpaka nafasi ya 7 kwenye msimamo wa Ligi na kujikusanyia alama 12.

Mchezo huu unategemewa kuwa mgumu hasa kwa upande wa Coastal Union walioshinda mchezo mmoja pekee katika Michezo mitano iliyopita.

Hivi ndivyo Yanga walivyotimba Dodoma






Post a Comment

0 Comments