UEFA: ARSENAL ,JUVE NA MAN CITY ZAPETA ,MADRID CHALI

 Michuano ya ligi ya mabingwa ulaya imeendelea usiku wa jana kwa raundi ya 6 iliyopigwa kwenye viwanja mbalimbali barani ulaya, mchezo uliokuwa unasubiriwa kwa hamu ni Manchester City wakikaribishwa Santiago Bernabeu na Real Madrid .





Haaland amaliza ufalme wa Mbappe Bernabeu

Manchester City wakiwa ugenini walifanikiwa kuondoka na ushindi wa mabao 2-1.  Mabao ya Nico OReiily na Mkwaju wa penati ya Haaland uliwafanya wenyeji kupigwa na butwaa.Matokeo hayo yanawafanya City kufikisha alama 13 sawa na PSG kwneye msimamo wa Ligi na sasa wapo nafasi ya 4.

Real Madrid imeshuka nafasi 1 na sasa ipo nafasi ya 7 wakiwa na alama 12 Inter Milan,Liverpool na Atletico Madrid.

Arsenal yaibagaza Club Brugge

Arsenal wameendelea kufanya vyema katika michuano hiyo baada ya kupata ushindi wa mabao 3-0 wakiwa ugenini.Shukrani za kipekee ziwaendee Nuno Madueke aliyepachika mabao 2 dakika ya 25 na 47 na Martinneli aliyepachika bao la tatu dakika ya 57. Ushindi huo unaifanya Arsenal kuongoza msimamo wa Ligi ya Mabingwa wakiwa na alama 18 katika mechi 6 walizocheza wakifungwa bao 1 na kufunga mabao 17.

Juventus waibamiza Pafos 

Juventus imeamka usingizini baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2=0 dhidi ya Pafos ,Mabao ya Juventus yaliwekwa kimiani na     Weston Mckennie dakika ya 67 na Jonathan David dakika ya 73.Ushindi hu unawafanya Juve kufikisha alama 9 katika mechi 6 walizocheza na kusimama nafasi ya 17 kwenye msimamo wa ligi.

Benfica wanasaka nafasi ya mtoano kinguvu. 

Matumaini ya kupata nafasi ya mchujo yameanza kuonekana kwa Benfica baada ya kushinda mechi mbili mfululizo. Katika mechi 4 za awali Benfica waliambulia vipigo lakini ushindi wa pili mfululizo dhidi ya Napoli umewafanya kufikisha alama 6 wakiwa nyuma ya Copenhagen FC na kama watashinda mechi mbili zijazo wanaweza kupata nafasi ya kucheza mtoano . 

Lwa upande wa Napoli SC wao wanahali mbaya baada ya kukubali kipigo hicho , Kwa sasa wana alama 7 kwenye msimamo wa ligi na wamekuwa na mwenendo wa kusuasua baada ya kucheza michezo 5 kuruhusu vipigo viwili,sare 1 na ushindi mechi 2.

PSG na Athletic Bilbao zavutana shati

Klabu ya Athletic bilbao imeshindwa kutamba uwanja wa nyumbani kwa kulazimishwa sare ya bila kufungana. Matokeo hayo yana faida kwa PSG ambao wamejikusanyia alama 13 kaatika michezo 6 na sasa wanakaa nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi ya mabingwa ulaya.



Post a Comment

0 Comments