ARSENAL WAUKARIBIA UBINGWA WA EPL

 Klabu ya Arsenal imeendelea kujihakikishia kutwaa ubingwa wa EPL baada ya kupata alama 1 dhidi ya Nottingham forest na kufikisha alama 50 kwenye msimamo wa Ligi.

Arsenal wamefikisha alama 50 katika michezo 22 waliyocheza mpaka sasa wakishinda Michezo 15 sare 5 na kupoteza Michezo 2 pekee. Wapinzani wao wa Karibu ni Manchester City  wenye alama 43 Sawa na Aston villa.

Kikosi cha Mikel Arteta kimekuwa kikifanya vizuri katika mashindano wanayoshiriki kuanzia UEFA ambako hawa

 I'lljapoteza mchezo wowote na wanaongoza msimamo wa Ligi,Michuano ya EFL(Kombe la Ligi) wapo Nusu fainali na watavaana na Chelsea Mzunguko wa pili baada ya kushinda Michezo wa Kwanza kwa mabao 3-2 ugenini Stamford bridge.

Maajabu ya soka la Uingereza 

Manchester city walipaswa kushinda mchezo dhidi ya Manchester United na kufikisha alama 46 hivyo kupunguza gepu la alama 7 dhidi ya wapinzani wao Arsenal. Kupoteza kwa mabao 2-0 dhidi ya majirani zao kumewahakikishia Arsenal kuweka m atumaini kuelekea mbio za ubingwa.

Hali hiyo imewakumba Aston villa ambao walipaswa kushinda mchezo dhidi ya Everton na kupanda mpaka nafasi ya pili wakiwa na alama 46 lakini na wao wamepoteza mchezo huo kwa bao 1-0 na kusalia nafasi ya 3 wakiwa na alama 43.Matokeo ya Manchester City na Aston villa yameleta faraja kwa Mashabiki wa Arsenal na sasa wameweka matumaini ya kubeba EPL baada ya kulikosa kombe Hilo kwa Miaka 22.

Kocha Liam Rosenior ameanza kwa kishindo EPL 

Matumaini ya kufanya vyema kwa Chelsea yameanza kuonekana baada ya kocha mpya Liam Rosenior kuiongoza timu hiyo kushinda kwa mabao 2-0 dhidi ya Bournemouth katika mchezo wake wa Kwanza wa EPL.

Kocha huyo raia wa Uingereza amekwishaiongoza Chelsea katika Michezo mitatu na kufanikiwa kushinda miwili huku akipoteza mmoja.

Ushindi mabao 5-0 dhidi ya Charlton katika mchezo wa FA kulileta faraja kwa Mashabiki wa Chelsea na alifanikiwa kufuzu raundi ya 4 watakapoumana na Hull city. Mchezo wa pili dhidi ya Arsenal Liam alipoteza kwa mabao 3-2 katika Nusu fainali ya Carabao Cup lakini ana nafasi ya kurekebisha makosa yake katika mchezo wa marudiano katika dimba la Emirates na kuipeleka Chelsea fainali.

Falsafa Yake ya 3-4-2-1 inaonekana kuleta tija kwa miamba hiyo ya London na amepewa kandarasi ya miaka 6 mpaka mwaka 2032 .


Post a Comment

0 Comments