Klabu ya Manchester United inapaswa kufanya maamuzi magumu yenye tija kwa kikosi Chao kuelekea msimu ujao wa 2026/27. Maamuzi hayo ni kumrejesha Mason Greenwood na Rashford walioondolewa ndani ya kikosi hicho. Nyota hao kwa pamoja wakiwa ndani ya United walifanikiwa kufunga jumla ya mabao 173 na kuipa klabu hiyo makombe ya EFL,FA na Europa League na kuisaidia timu hiyo kucheza michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya
Kwanini Mason Greenwood arejeshwe kikosini?
Manchester United wanakabiliwa na changamoto ya eneo la ufungaji na hiyo ilipelekea msimu wa 2024/25 kumaliza nafasi ya chini na kushindwa kufuzu Uefa.Sajili za Benjamin Sesko,Bryan Mbeumo,Matheus Cunha bado hazijazaa matunda mpaka sasa kutokana na nyota hao kufunga jumla ya mabao 16 katika mechi zote walizocheza msimu huu.
Msimu wa 2024/25 Greenwood aliuanza vyema akiwa na jezi ya Olympic Marseille akipachika mabao 21 katika Michezo 34 Ligue 1 na kuwa mfungaji bora sawa na Osman Dembele mshindi wa Ballon d'Or pamoja na FIFA Men's bestplayer.Wengi walidhani Greenwood alibahatisha.
Msimu wa 2025/26 nyota huyo ameendelea kufanya vyema Ligue 1 baada ya kupachika mabao 11 katika Michezo 16 na ameendelea kuwa kinara wa ufungaji wa Ligi hiyo. Mbali na Hilo Greenwood ameweka rekodi ya kipekee ndani ya Olympic Marseille akipachika Jumla ya mabao 41 katika Michezo 61 aliyocheza.
Rashford ni muhimu zaidi kikosini kwa sasa
Marcos Rashford amekuwa lulu ndani ya kikosi cha Barcelona tangu kusajiliwa kwake kwa mkopo. Nyota huyo ameshacheza jumla ya mechi 28 akifunga mabao 7 na kutengeneza mengine 11 na kumfanya kuchangia jumla ya mabao 18 katika mechi 28 sawa na wastani wa 0.5 katika kila mechi anayocheza.
United wanamuhitaji zaidi Rashford kutokana na kiwango bora anachokionyesha Barcelona ukilinganisha na wachezaji waliopo klabuni hapo.
Uwepo wa Michael Carrick ni tija kwa United
Michael Carrick ni legend ndani ya United na sasa amekabidhiwa mikoba ya kuinoa United mpaka mwishoni mwa msimu akichukua nafasi ya Ruben Amorim aliyetimuliwa kutokana na mwenendo mbaya wa timu hiyo. Ushawishi alionao unaweza kuwarejesha Marcos Rashford na Mason Greenwood ndani ya kikosi chake kwa msimu ujao lakini pia anaweza kutumika kuwavuta nyota wengine bora ndani ya United.



0 Comments