Barcelona wameendelea kufanya vyema mbele ya Real Madrid baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 3-2 katika fainali za kombe la Supercopa de Espana.
Shukrani za kipekee zimwendee mbrazil Rafinha aliyepachika mabao 2 na kuibuka nyota wa mchezo huku bao la 3 kwa Barcelona likiwekwa kimiani na mkongwe Roberto Lewandowski.Real Madrid walipata mabao yao mawili kupitia kwa Vinicius Jr na Garcia.
Barcelona wameendelea kuwa wababe wa Kombe la Supercopa Espana wakifanikiwa kutwaa taji Hilo mara 16 wakifuatiwa na Real Madrid wenye taji Hilo mara 13. Awali michuano hiyo ilihusisha timu mbili pekee kwa maana ya mshindi wa Copa del Rey dhidi ya mshindi wa La Liga na mfumo huo ulidumu mpaka mwaka 2020 ambapo timu nne zilianza kushiriki michuano hiyo.
Hans Flick ageuka mwiba mkali kwa Real Madrid
Kocha Hans Flick ameendelea kuwa mwiba mkali kwa Real Madrid akiweka rekodi ya kushinda Michezo 4 na kufunga mabao 16 huku akiruhusu mabao 7 na kuisaidia klabu hiyo kutwaa makombe ya Copa De Rey msimu wa 2024/25 na sasa Supercopa Espana.
Kwa upande wa La Liga Hans Flick ameendelea kuwa Moto wa kuotea mbali baada ya kuisaidia Barcelona kukaa kileleni ikiwa na alama 49 baada ya kushinda Michezo 16 sare 1 na kupoteza Michezo 2 huku akiwaacha Real Madrid kwa alama 4.
Kocha huyo ameendelea kufanya vyema kombe la Copa del Rey na atavaana na Racing katika hatua ya 16 bora. Kombe linalompa wakati mgumu kocha huyo ni Ligi ya Mabingwa ulaya (UEFA) ambako wanashika nafasi ya 16 wakiwa na alama 10 pekee katika Michezo 6.

0 Comments