HESABU ZA SIMBA KWENDA ROBO FAINALI NINGUMU ILA ZINAPIGIKA

 Klabu ya Simba imeendelea kufanya vibaya hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Africa baada ya kukubali kipigo cha bao 1-0 dhidi ya Esperance matokeo yaliyowafanya Simba kusalia mkiani mwa kundi D wakiwa na alama 0. Huu ni msimu mbaya zaidi kwa Simba toka mwaka 2018 ilipoanza kufanya vyema Michuano hiyo.kufungwa mechi tatu mfululizo kumeibua sintofahamu miongoni mwa Mashabiki wakiwataka viongozi kutafuta suluhu ya migogoro na kuirejesha timu pamoja kuelekea raundi ya pili ya Michuano hiyo.

"Kufungwa mechi tatu ni Jambo baya kwa klabu kubwa kama Simba lakini tunaweza kupindua meza raundi ya pili"
"Tumefanya sajili za wachezaji wenye uwezo na uzoefu wa Michuano ya kimataifa na Jambo kubwa zaidi tuna michezo miwili ya hapa nyumbani dhidi ya Stallen Borch na Esperance de Tunis .tunatakiwa kushinda mechi hizo kwa namna  yoyote na kupata alama 6 kisha kuhakikisha tunashinda mechi ya ugenini dhidi ya Petro de Luanda pale Angola ."
"Kwa uzoefu wetu wa hii Michuano ni fedheha Sana kumaliza kwa hatua ya makundi tena katika nafasi hizi mbaya,tunataka kwenda fainali kama tulivyofanya msimu uliopita Michuano ya Kombe la shirikisho" -maneno ya kiongozi wa Simba aliyekataa kutajwa jina lake.

NAMNA SIMBA WANAVYOWEZA KUFUZU HATUA YA MAKUNDI
Kundi D linaongozwa na Stallion de mallin wakiwa na alama 7 nafasi ya pili ni Esperance wenye alama 5 ,Petro de Luanda Wana alama 4 na Simba alama 0.,kama Simba atashinda mechi zote tatu atakuwa na alama 9 na kufanikiwa kushika nafasi ya 2. Wakati huo ataomba vilabu   Esperance na Petro de Luanda vitoke sare ili na kufungwa na Stallion de Mallin.

Post a Comment

0 Comments