Klabu ya Arsenal imefanikiwa kutinga fainali za EFL baada ya kuibuka na ushindi mnono wa mabao 3-2 dhidi ya Chelsea.

Katika mchezo huo mkali uliopigwa dimba la Stamford Bridge uliishuhudia Arsenal ikipata bao la uongozi dakika ya 7 kupitia kwa Ben White na Gyokeres alifunga bao la pili dakika ya 49 . Chelsea walirejea mchezoni dakika ya 57 kupitia kwa  Garnacho lakini Arsenal walipigilia msumari wa bao la tatu kupitia kwa Zubimendi dakika ya 71. Bao la pili kwa Garnacho dakika ya 83 halikutosha kuiokoa Chelsea na kuipeleka fainali.

Kwa upande wa Arsenal wameendelea kuwa na mwaka Bora wa mashindano baada kutinga fainali za EFL,kuongoza msimamo wa UEFA na EPL.

ALONSO AKALIA KUTI KAVU REAL MADRID 

Klabu ya Real Madrid imeendelea kuwa na wiki mbaya baada ya kuondoshwa kwenye michuano ya Copa del Rey hatua ya 16 bora dhidi ya Albacete Madrid walipoteza mchezo huo kwa jumla ya mabao 3-2. 

Huu ni mchezo wa pili mfululizo kwa Real Madrid kupoteza ndani ya wiki moja baada ya mchezo wa fainali ya Super copa Espana dhidi ya Barcelona waliopoteza kwa mabao 3-2 .

Kocha Xabi Alonso ameendelea kukalia kavu kwa matokeo mabaya ya mechi huku wachezaji wengi wakipinga falsafa anazotumia kufundisha na kuiboresha timu hiyo. 

Maelewano mabovu baina ya Alonso na wachezaji yameendelea kuiangamiza Real Madrid naa kuna uwezekano akafukuzwa hapo baadaye 



Post a Comment

0 Comments