Tumefanya tathmini ya makocha hawa na namna wanavyokwenda kuleta mwanzo mpya ndani ya Vilabu
Michael Carrick -Manchester United
Kocha Michael Carrick ni Legend ndani ya Manchester United amehudumu kama mchezaji kisha kocha wa mpito na baadaye alipelekwa timu ya Vijana na sasa amekabidhiwa mikoba ya kuiongoza United mpaka mwisho wa msimu.
Kibarua cha Kwanza kwa Carrick ilikuwa mchezo mgumu wa Ligi dhidi ya wapinzani wao Manchester City na kwa bahati nzuri alishinda mchezo huo na kuleta faraja kwa waajili wake pamoja na Mashabiki wa United.
Kocha huyo ataiongoza United katika Michezo 16 na Jambo pekee analopaswa kulifanya ni kuhakikisha United inafuzu kucheza Ligi ya Mabingwa ulaya kwa msimu wa 2026-27 .
Liam Rosenior -Chelsea
Kusuasua kwa Chelsea kulipelekea bodi ya wakurugenzi chini ya Toddy kumleta Liam ili kuokoa jahazi lililokuwa linapaswa kuzama. Kocha Liam Rosenior ameiongoza Chelsea katika Michezo 3 akishinda 2 na kupotezachezo mmoja.
Mashabiki wameanza kumuelewa kocha huyo kijana mwenye miaka 41 na amepewa mkataba wa kukaa klabuni hapo mpaka mwaka 2032 kama atafanya vyema ikiwemo kutwaa ubingwa wa Ligi kuu,Fa na carabao cup na kuhakikisha timu hiyo inashiriki Ligi ya Mabingwa ulaya kila msimu.
Falsafa Yake ya 3-4-2-1 inaonekana kuwakonga wachezaji wa Chelsea hasa katika mchezo dhidi ya Brentford ambao Chelsea waliibuka na ushindi wa mabao 2-0
Arbeloa Alvaro -Real Madrid
NI legend ndani ya Real Madrid na anakumbukwa kwa uwezo wake akicheza nafasi ya beki wa kulia. Nyota huyu amechukua nafasi ya Xabi Alonso ambaye ameondoshwa klabuni hapo baada ya kuwa na msimu mbaya ndani ya klabu Kama kocha.
Kiu kubwa ya Real Madrid ni kutwaa ubingwa wa La Liga na UEFA msimu huu kutokana na umahili wa wachezaji waliopo kikosini kama Kylian Mbappe, Vinicius Jr ,Jude Bellingham na Diaz.
Mchezo wa kwanza kwa Alvaro Arbeloa kama Kocha alifanikiwa kushinda kwa mabao 2-0 dhidi ya Levante na hiyo ilipelekea Mashabiki kujenga Imani naye.
Ushindi huo uliifanya Real Madrid kufikisha alama 48 nyuma ya vinara Barcelona wenye alama 49.Usiku wa Leo Alvaro Arbeloa ataiongoza tena Real Madrid katika mchezo dhidi ya Monaco NI mchezo muhimu na unapigwa Santiago bernabeu hivyo Madrid wanapaswa kushinda kwa namna yoyote.




0 Comments