UNAI EMERY NA GUARDIOLA WAFURAHISHWA NA CUNHA KUHARIBU MBIO ZA MBIO ZA UBINGWA KWA ARSENAL

Utamu wa Ligi kuu ya Uingereza (EPL) umeendelea wikiendi hii na mechi kubwa iliyokuwa ikisubiriwa na Mashabiki hasa wa Arsenal na Manchester City ni mechi ya Arsenal akiwa nyumbani Emirates dhidi ya Manchester United iliyo chini ya Michael Carrick.

Hamu ya Mashabiki ni kujua muafaka wa timu zao katika mbio za ubingwa ambao kwa sasa upo mzunguko wa pili raundi ya 23 na wanatambua kupata au kupoteza point kutaamua hatma ya bingwa wa msimu wa 2025/26
Raundi ya 22 tuliishuhudia Manchester City ikipoteza mchezo wake dhidi ya Manchester United kwa mabao 2-0  Arsenal wao walipata sare ya 0-0 dhidi ya Brighton na hii iliwapa nafasi nzuri Arsenal kusalia kileleni kwa kujiamini wakiongoza Ligi kwa tofauti ya alama 7 dhidi ya Manchester city pamoja na Aston villa ambao nao walipoteza kwa bao 1-0.
Raundi ya 23 mambo yamekuwa mazuri kwa  Aston villa wakipata ushindi WA mabao 2-0 dhidi ya Newcastle United na upande wa Manchester city wakipata ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Wolves na wote  kufikisha alama 46,  huku Arsenal wakikubali kipigo cha mabao 2-3 dhidi ya Manchester United na kusalia kileleni wakiwa na alama 50.
Tathmini ya mchezo wa Manchester United Vs Arsenal
Arsenal chini ya kocha Mikel Arteta walipata bao la kuongoza dakika ya 29 kupitia kwa beki wa Manchester United Laurato Martinez lakini bao Hilo lilidumu mpaka dakika ya 37 ambapo Mshambuliaji Mbeumo aliisawazishia United na kwenda mapumziko kwa Sare ya 1-1.
United walipata bao la pili dakika ya 50 kupitia kwa Dorgu lakini Merino wa Arsenal alisawazisha bao Hilo dakika ya 84. Dakika ya 87 United walipata bao la tatu na la ushindi kupitia kwa winga Mathew Cunha na kuwanyamazisha Arsenal.
Hatma ya ubingwa kwa msimu huu
Mpaka sasa hakuna timu iliyojihakikishia kutwaa ubingwa msimu huu. Kuna makundi mawili yanayopigiwa chapuo mpaka sasa,kundi la Kwanza linaundwa na Timu za Arsenal chini ya Mikel Arteta wana alama 50 ,Aston villa chini ya Unai Emery na Manchester city chini ya Pep Guardiola wana alama 46 tofauti ya alama 4 pekee.Timu hizi ndizo zinazopewa nafasi kubwa ya kutwaa ubingwa  kutokana na kujikusanyia alama za kutosha.
Kundi la pili linaundwa na Manchester United chini ya Michael Carrick, Chelsea chini ya Liam  na Liverpool chini ya Arne Slot. Timu hizi zinakwenda kwa kusuasua na hazipewi nafasi ya kushinda ubingwa bali kukwamisha au kuamua hatma ya bingwa wa msimu huu. Kundi hili linapigana Kufa na kupona kuhakikisha timu zake zinasalia nafasi nne za juu.

Post a Comment

0 Comments