MATUMAINI YA RONALDO YAZIMWA NA AL HILALA

Matumaini ya Cristiano Ronaldo kutwaa a kombe la Ligi kuu ya Saudia (Saudi Pro League) yameanza kupotea msimu huu baada ya kufanya vibaya mechi 4 mfululizo.



Michezo 10 ya mwanzo wa Ligi Al Nassr walishinda na kujikusanyia alama 30 lakini Michezo minne iliyofuata wameambulia pointi Moja pekee baada ya kukubali sare ya mabao 2-2  dhidi ya Al Ittifaq kisha kupoteza kwa mabao 3-2 dhidi ya Al ahli Saudi mchezo wa ugenini kisha kupoteza kwa mabao 2-1 dhidi ya Al Qadisia na kipigo cha bao 3-1 dhidi ya Al Hilal kimeharibu kila kitu

Matokeo hayo yamewapeleka Al Nassr mpaka nafasi ya 2 nyuma ya Al Hilal 38 katika Michezo 14 na sasa wanatofauti ya alama 7.

Ujio wa João Felix unatija kwa Al Nassr ?

Usajili wa João Felix ndani ya Al Nassr NI faida kwa timu kwani nyota huyo amefanikiwa kufunga Jumla ya mabao 13 katika mechi 14 za Saudi Pro League na ndiye anayeshika nafasi ya pili nyuma ya Ronaldo mwenye mabao 15.

Al Nassr imefunga Jumla ya mabao 39 katika mechi 14 na kuwa timu inayoongoza kwa mabao katika Ligi Sawa na Al Hilal yenye mabao 39. Nyota hao wawili wa kireno  wamepachika Jumla ya mabao 28 Kati ya 39 ya Al Nassr 

Post a Comment

0 Comments