Mashabiki wa Simba wameendelea kukosa utulivu kutokana na mwenendo mbaya wa timu hiyo hasa Ligi kuu baada ya kupoteza alama 2 muhimu dhidi ya mtibwa Sugar katika mchezo wa raundi ya 5 uliopigwa dimba la Meja Isamuyo Bunju.
Maumivu ya Simba yalianza Ligi ya Mabingwa Africa kwa kupoteza Michezo miwili ya awali kisha kupoteza Mchezo wake wa Kwanza wa Ligi kuu dhidi ya Azam FC mchezo uliomalizika kwa kipigo cha mabao 2-0. Azam FC waliiondosha tena Simba katika Michuano ya Mapinduzi Cup kwa bao 1-0.
Tathmini ndogo inaonyesha Simba imepoteza Michezo 3 sare 1 na kushinda 1 katika Michezo 5 waliyocheza ya Ligi kuu pamoja na Ligi ya Mabingwa.
Muarobaini wa kurejesha utulivu ndani ya Simba umepatikana
Waswahili husema yaliyopita si ndwele tugange yajayo na hiyo ndio kauli wanayotakiwa kubeba viongozi,Mashabiki pamoja na wachezaji wa Simba.
Kupoteza mechi nyingi katika kipindi kifupi huharibu malengo ya timu.
1.Simba watakaribishwa nchini Tunisia kuvaana na Esperance de Tunis katika mchezo wa raundi ya tatu ya Ligi ya Mabingwa Africa na wanapaswa kushikamana na kushinda mchezo huo ili kurejesha matumaini ya kufuzu robo fainali kwani kupoteza Mchezo huo kutaharibu mipango ya timu na kuvuruga Amani ndani ya klabu.
2.Mbali na ushirikiano baina ya viongozi,Mashabiki na wachezaji suala la usajili ndiyo mkombozi wa Simba. Kila eneo la Simba linahitaji maboresho. Sajili zisiwe za kuokoteza wachezaji bali waje wachezaji wenye uwezo mkubwa watakaoleta changamoto kwa wachezaji waliopo kwa sasa.
3.kocha na benchi la ufundi wapewe ushirikiano wa kutosha nyakati hizi. Ushirikiano si kuingilia majukumu yake bali kumpa ushirikiano utakaoleta tija ndani ya timu. Nidhamu kwa wachezaji na viongozi kutaleta changamoto chanya kwa timu.

0 Comments