DEMBELE AFANYA YAKE KUIREJESHA PSG KILELENI

 Mabao mawili yaliyofungwa na Ousmane Dembele yalikamilisha ushindi mnono wa mabao 3-0 dhidi ya Lille na kuirejesha PSG kileleni mwa Ligue 1 ikiwa nyumbani katika dimba la Parc des Princes.

Dembele amekuwa nje ya uwanja na kukosa baadhi ya mechi hapo awali lakini alirejea kwa kishindo na kufanikiwa kupachika bao la Kwanza dakika ya 13 na bao la pili dakika ya 64 huku Bradley Barcola akipachika bao la tatu dakika ya 90+3.

Kocha Luis Enrique aliwaanzisha Dembele,Desire Doue na Kvaratskhelia katika Safu ya ushambuliaji Sawa na alivyoanza katika Michezo wa fainali dhidi ya Inter Milan katika Michezo wa fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya mwezi mei na katika kikosi hicho alikosekana Achraf Hakimi anayeshiriki AFCON nchini Morocco na siku ya jumapili ataiongoza timu hiyo dhidi ya Senegal.

Ushindi muhimu dhidi ya Lille

Kocha Luis Enrique alitambua umuhimu wa ushindi wa mchezo dhidi ya Lille kutokana na Ushindani uliopo katika Ligi ya Ufaransa.

Klabu ya Lens RC ndiyo wapinzani wakuu kwa PSG msimu huu wakicheza Michezo 17 wakishinda 13 ,sare 1 na kupoteza Michezo 3 pekee huku wakiwa na alama 40 nyuma ya PSG wenye alama 42 wakicheza Michezo 18.

Mchezo unaofuata kwa RC LENS ni dhidi ya AJ Auxerre kama Lens watashinda mchezo huo watapaa kileleni na kuwazidi PSG kwa alama 1 na kuanza Mzunguko wa pili wa Ligue 1 kwa kishindo.Ikumbukwe Lens wamekuwa Bora katika Michezo mitano iliyopita wakishinda mechi zote. 

Msimu wa 2024/25 PSG walitwaa ubingwa wa Ligue 1 wakiwa na alama 84 nafasi ya pili ilikuwa ni Olympic Marseille wakiwa na alama 65 Sawa na tofauti ya alama 19. 

Msimu huu mambo yamebadilika na vilabu vya RC Lens , Olympique de Marseilles,Lille na Olympique Lyon vimekuwa vikileta ushindani.

Je Dembele atatetea kiatu chake cha Dhahabu?

Ni swali gumu kuweza kujibuka kwa sasa kwani nyota huyo amefunga mabao 5 katika mechi 10 za Ligue 1 kwa msimu huu. Nyota huyo amekuwa akikumbwa na majeraha ya mara kwa mara na hii imepelekea kukosekana kwenye baadhi ya mechi.

Mason Greenwood anaongoza mbio za ufungaji akiwa na mabao 11 katika mechi 16 Sawa na tofauti ya mabao matano baina ya nyota hao ambao msimu uliopita wote walimaliza wakiwa na mabao 21.

Kama Dembele arejea vyema katika majeraha yake basi mbio za ufungaji Bora bado ziko wazi ikizingatiwa anamichezo 16 ya raundi ya pili ya Ligue 1


Post a Comment

0 Comments