Mbio za ufungaji Bora barani ulaya zimeendelea kushika Kasi na sasa nyota watatu wanatajwa kuwania kiatu cha Dhahabu cha ulaya.Msimu wa 2024/25 majina ya Mbappe ,kane na Halaand yalijitokeza lakini Mbappe aliinuka kinara na kuwabwaga wapinzani wake hao na kutwaa kiatu hicho akifunga Jumla ya mabao 31.
Msimu wa 2025/26 mbio hizo zinaongozwa na Harry Kane aliyefunga Jumla ya mabao 22 mpaka sasa akifuatiwa na Halaand mwenye mabao 21 na Mbappe mwenye mabao 19. Ikumbukwe mabao yanayohesabiwa hapa NI Yale yaliyofungwa katika Ligi kuu pekee na si Michuano mwingine.
La Liga inaongozwa na Mbappe mwenye mabao 19 katika Michezo 19 aliyocheza. EPL inaongozwa na Halaand mwenye mabao 21 katika Michezo 22 na Harry Kane akiwa na mabao 22 katika Michezo 22.
Ushindani wa nyota hao umezidi kunoga kuelekea kombe la dunia nchini Marekani ambapo watatazamwa kama wakombozi WA timu zao za taifa za Ufaransa kwa Mbappe,Norway kwa Halaand na England kwa Harry Kane.

0 Comments