Kocha anayeondoka Crystal Palace, Oliver Glasner, ni miongoni mwa majina yanayozingatiwa kuchukua nafasi ya ukocha wa Manchester United msimu wa joto ujao. (Mirror)
Chelsea na Manchester City wanaongoza katika mbio za kumsajili kiungo mshambuliaji wa Barcelona, Mhispania mwenye umri wa miaka 18 Dro Fernandez, ambaye ana kipengele cha kuachiliwa cha pauni milioni 5.1 (euro milioni 6) katika mkataba wake. (Talksport)
Kocha wa Tottenham, Thomas Frank, anataka kumsajili mchezaji wa kushambulia upande wa kushoto, ama mwezi Januari au majira ya joto. (Telegraph)
Kiungo wa England James Ward-Prowse, 31, anaweza kuondoka West Ham, huku Burnley wakionyesha nia ya kumsajili nahodha wa zamani wa Southampton. (Sun)
Leeds United wameulizia upatikanaji wa mshambuliaji wa Norway Jorgen Strand Larsen, 25, lakini bado hawajatoa ofa rasmi kwa Wolves. (Athletic)
Inter Milan wanapanga kumpa mkataba mpya mshambuliaji wa Italia mwenye umri wa miaka 20 Francesco Pio Esposito, ili kuzima nia ya vilabu vya Ligi Kuu ya England. (Tuttosport)
Crystal Palace wako hatarini kumpoteza mchezaji mwingine muhimu, huku mshambuliaji wa Ufaransa Jean-Philippe Mateta, 28, akiwa tayari kwa changamoto mpya na Juventus wakionyesha nia ya kumnyakua. (Sky Sports)

Real Madrid wataanza mazungumzo ya mkataba mpya na mshambuliaji wa Brazil Vinicius Jr, 25, kufuatia kuondoka kwa Xabi Alonso katika uwanja wa Bernabeu. (ESPN)


0 Comments