YANGA WAREJEA KILELENI KIBABE NA HIZO NI SALAMU KWA AL AHLY

 Klabu ya Young Africans imeendelea kufanya vyema Ligi kuu ya NBC baada ya kuibuka na ushindi mnono wa mabao 6-0 dhidi ya Mashujaa FC katika dimba la nyumbani KMC COMPLEX 

Katika mchezo huo uliokuwa wa kuvutia uliishuhudia Yanga ikipata bao la uongozi kupitia kwa Damaro dakika ya 8,bao la pili likiwekwa kimiani naDuke Abuya dakika ya 28 ,bao la tatu likiwekwa kimiani na Pacome Zouzoua na kwenda mapumziko wakiwa mbele kwa mabao 3-0.

Kipindi cha pili kilirejea na Prince Dube aliachika bao la nne dakika ya 79 ,bao la tano likiwekwa kimiani na Mudathir Yahya dakika ya 81 na bao la Sita likiwekwa kimiani na Depu dakika ya 90 .

Matokeo hayo yameipeleka Yanga kileleni mwa msimamo wa Ligi kuu ya NBC ikiwa na alama 19 katika Michezo 7 waliyocheza wakishinda Michezo 6 na sare 1.

Jambo la kipekee kwa Yanga msimu huu NI kufunga Jumla ya mabao 18 wakiruhusu bao Moja pekee katika Michezo 7.

Yanga watuma salamu Al Ahly 

Ushindi WA mabao 6-0 NI salamu kwa Al Ahly kuelekea mchezo wa makundi ya Ligi ya Mabingwa Africa mchezo utakaopigwa nchini Misri tarehe 23 Januari na Yanga wanapaswa kushinda mchezo huo muhimu ili kujiweka sawa katika kundi B ambako wanashika nafasi ya pili wakiwa na alama 4 Sawa na Al Ahly.

Kundi hilo linaundwa na vilabu vya Al Ahly,Yanga,Js Kablyie,na As Far . Kama Yanga watapata alama katika mchezo huo watajiweka katika mazingira mazuri ya kufuzu robo fainali ya Michuano hiyo.


Post a Comment

0 Comments