AL NASSR WAKARIBIA KILELENI BILA CRISTIANO RONALDO

 Ligi kuu ya nchini Saudi Arabia (roshn pro League) imeendelea kuwa Moto baada ya Al Nassr kushinda mchezo dhidi ya Al Ittihad kwa mabao 2-0. Shukran za kipekee ziwaendee Sadio Mane aliyepachika bao la uongozi dakika ya 84 kwa mkwaju wa Penati na bao la kihisia kutoka kwa Angelo Gabriel dakika ya 90+6.

Matokeo hayo yamewapeleka Al Nassr mpaka nafasi ya pili wakiwa na alama 49 nyuma ya vinara Al Hilal  wenye alama 50 katika Michezo 20 nafas nafasi ya tatu inashikiliwa na Al Ahli wenye alama 47 katika Michezo 20.

Sababu za Cristiano Ronaldo kukosekana dhidi ya Al Ittihad
Wiki hii kuliibuka mgongano baina ya mchezaji Cristiano Ronaldo na uongozi wa Ligi hiyo akiwatuhumu kwa kupendelea baadhi ya Vilabu kama Al Hilal na Al Ittihad na kupelekea klabu yake ya Al Nassr kushindwa kutwaa kikombe chochote tangu alipojiunga na miamba hiyo mwaka 2022 akitokea Juventus.Tuhuma hizo zilipelekea Ronaldo kujitenga na kambi ya timu katika mechi mbili zilizofuata ukiwemo mchezo muhimu dhidi ya Al Ittihad.
Uongozi wa Ligi hiyo umejitetea kuhusu tuhuma hizo wakisema kila klabu ina misingi yake ya kiuendeshaji na namna wanavyoweza kusajili mchezaji yeyote na wao kama bodi ya ligi wanajukumu la kuhakikisha timu zinafuata miongozo na kanuni zilizowekwa na si kupanga nani awe bingwa msimu huu.
Sakata hili bado lamoto na limefungua Milango ya Ronaldo kutaka kuondoka Saudi Arabia mwezi June endapo madai Yake hayatasikilizwa na kufanyiwa kazi.
Mbio za kiatu cha Dhahabu zageuka gumzo
Ukiachana na vita ya Ubingwa,madai ya Cristiano Ronaldo vita nyingine ni Ile ya kumpata Mfungaji bora wa Ligi hiyo. Mwanzoni mwa msimu wa Ligi hiyo washambuliaji Cristiano Ronaldo na João Felix walikuwa Moto wakiongoza orodha ya ufungaji na kupewa nafasi kubwa ya kutwaa kiatu cha Dhahabu
Kwa sasa mambo yamebadilika na majina ya Ivan Toney na Julian Quinones yameibuka na kuwa gumzo jipya katika Ligi hiyo.Mshambuliaji Julian Quinones kutoka Al Quidsiah amefunga mabao 17 idadi Sawa na Cristiano Ronaldo na wote wako nafasi ya pili nyuma ya Ivan Toney mwenye mabao 19 katika Michezo 19 aliyocheza mpaka sasa.
Mshambuliaji Ivan Toney kutoka Al Ahli amewakosha Mashabiki wa Ligi hiyo kutokana na uwezo wake wa kufunga kwa mashuti ya mbali na spidi anapokuwa na mpira na chenga zake za maudhi kwa wapinzani wake. Migogoro ya Ronaldo na Bodi ya Ligi ya Saudia Unampa nafasi Ivan kujiwekea mazingira mazuri ya kutwaa kiatu hicho cha Dhahabu .

Post a Comment

0 Comments