Swali hili Sio saizi yangu na nafikiri hata wenye saizi nalo huu Sio wakati wa kuulizana maswali tena ya namna hii.
Binafsi napenda kujibu swali la *_performance ya Simba imefikia wapi..???_
Well,Jana nilitazama mechi ya Simba v KMC ambayo iliisha Kwa Simba kuibuka na ushindi wa magoli 2-0 lakini pia walionyesha performance nzuri . Kwenye kuandaa timu kitu muhimu kabisa Cha kwanza kocha anadili nacho ni performance ya timu na Kuna muda utawasikia walimu wakihojiwa baada ya mechi _timu yangu imeshinda lakini sijaridhika na performance_ kumbe ni kweli inatakiwa ianze performance halafu ndio yafuate matokeo.
Simba Jana v mpinzani ambaye ni wa mwisho ktk msimamo wa NBC alionyesha performance nzuri na kupata matokeo hata hivyo hili Sio jambo dogo .! Na kwangu Mimi fafsiri yake ni matokeo ya benchi la ufundi na kiu ya mafanikio ikichagizwa na maingizo mengi mapya ya wachezaji ktk timu.
Miaka ya hivi karibuni Simba ilikuwa inaonekana ikisajili wachezaji wa kigeni ambao wengi walishindwa kuonyesha viwango na kuisaidia timu na hatimaye kuachwa muda mfupi tu baada ya kusajiliwa.
Simba ya Jana KMC inahitaji iachwe ikae muda wa kutosha pamoja isiruhusu zile ingia toka ingia toka zilizosababisha Kila msimu timu kuanza upya (hakuna muendelezo) na hii sio sifa ya timu kubwa badala yake viongozi wafanyie kazi kusajili maeneo yenye uhitaji maalumu lakini Sio kusajili karibu timu nzima Kila Msimu.
Nasema hv Kwa sababu usajili wa sasa wamekuja wachezaji wanaoendana na falsafa ya timu _lunyasi_ na wana vipaji vikubwa wakina Oura ,Loemba,Gueye ,Morice kiukweli _they are not JOBE_😊 Simba hii ikikaa pamoja muda wa kutosha sitashangaa ikifikia kiwango cha ile Simba ya _Miquisson_ timu zinafungwa na mpira zinachezewa.! achana na kipindi kile _pira objective_ mradi matokeo tuu.
*UCHAMBUZI KWA IDARA*
Hakuna mashaka makubwa sana eneo la _Goalkeeping_ Jana kadaka Abel lakini Kuna Yakoub na huu usajili mpya _no problem_.
Eneo la _Defending_ De Reuck ndio kiongozi pale na Toure ni tofauti kabisa na Kalaboue Shamou ambaye katoka Kwa sasa,Toure, kimo, utulivu,control , aggressiveness vinambeba.Kulia Kwa Kapombe ni kweli Kuna Kapombe lakini anahitajika kijana awe anaivizia ile nafasi naona Duchu jana na leo bado haonyeshi kuwa na matamanio hayo .Enzi hizo tungesema kushoto Kwa Shabalala ,sasa kuna Kibabage na Mligo wote hawa bado wanahukumiwa na kivuli Cha Muddy aliyetimkia upande wa pili,kwangu mimi wawili hawa hakuna aliyemwacha mwenzake mbali ila wote wako pungufu ya Shabalala.
Kagoma,Naby viungo eneo la ulinzi nao kwangu hakuna aliye mbali sana na mwenzie.
Semfuko Charles,Neo Maema,Morice Abraham jana alitumika eneo hili la kupeleka mashambulizi mbele kwa washambuliaji eneo hili kila mmoja atumike kwa uhitaji wa mechi husika bila kumsahau Semfuko Charles kipaji kikubwa aongezewe game time kiwanjani ⚽.Aura,Gueye, Loemba,Chama,Mpanzu, ukimtoa Chama hao wengine 4 _Steve Baker_ watumie pembeni kushoto au kulia _unavyopenda unavyotaka_.! Chama mwache shimoni eneo alilopatia umaarufu toka enzi,katikati ya ukuta wa timu pinzani na viungo wao mwache Chama aishi pale,mwache Chama apige pasi zake za mwisho 😊
*_SOWAH NA MWALIMU_*
Tangu mwanzo andiko langu halikuwakataza Simba kusajili ila nilishauri usajili huo ulenge eneo mahsusi.! Hawa washambuliaji wawili wana kazi ya kufanya ,na mpira ni mchezo wa wazi na wote tunaona.
Mwalimu kafunga jana(kanufaika na second ball) angeweza kufunga zaidi ila bado mikimbio yake hai match na akili za viungo wake washambuliaji anahitajika sana kuongeza utulivu mbele ya lango bila mpira na akiwa na mpira asiamini tu striker nguvu na mikimbio akasahau hesabu wakati Sowah anajitambulisha kama striker finisher ndani na karibu na box la mpinzani basi inabidi aachane na hasira hasa anapokuwa anadhibitiwa na mlinzi akubali asubiri nafasi afunge ndio jukumu lake.
Wote hawa wawili wanahukumiwa na vivuli vya J Bocco, M Kagere na C M Mugalu tukiwatizama tunajisemea moyoni _mbona Sio kama Bocco?_
Niliwahi washauri Simba waachane na kelele za milinganisho na mifanano ya wao na wapinzani wao wajikite ktk kutengeneza Simba mpya na inawezekana..!!
Kama tunalikubali hili 👆kubalini na hili
"*_MATOKEO YOYOTE YA MECHI YA DABI 1/3/2026 YASITUMIKE KAMA KIPIMO CHA UTENGENEZWAJI WA TIMU_*"
SIMBAAAAA
NGUVU MOYAAA🦁
Katembo +255 711 328383.

0 Comments