Manchester city wamefanikiwa kutinga fainali za Carabao Cup baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Newcastle United na kuwafanya kutinga fainali kwa Jumla ya mabao 5-2 baada yachezo wa Kwanza kushinda mabao 2-0.
Omary Marmoush aliibuka nyota wa mchezo huo akipachika mabao 2 dakika ya 7 na 29. Bao la tatu kwa City liliwekwa kimiani na T.Reijnder dakika ya 32. Newcastle United walipata bao la kufutia machozi dakika ya 62 kupitia kwa Antony Elanga
Manchester city watavaana na Arsenal katika fainali itakayopigwa Machi 1 katika dimba la Wembley Jijini London. Arsenal wamefika fainali hizo baada ya kuibuka na ushindi wa Jumla ya mabao 4-2 ya Chelsea. Mchezo wa Kwanza Arsenal walishinda kwa mabao 3-2 na mchezo wa pili walishinda kwa bao 1-0.
Manchester City na Arsenal wamekuwa na Ushindani mkali katika Michuano mbalimbali wanayoshiriki msimu huu kuanzia Ligi kuu ambayo Arsenal wanaongoza kwa alama 53 wakifuatiwa na Manchester city wenye alama 47 Sawa na tofauti ya alama 6 wote wakiwa wamecheza Michezo 24
Mchezo huu wa fainali umeibua hisia miongoni mwa Mashabiki wa soka hasa wakikumbuka namna Pep Guardiola alivyokuwa akimnoa Mikel Arteta kwa Miaka minne iliyopita. Mashabiki wengi wanaamini Arsenal wananafasi kubwa ya kubeba kombe Hilo msimu huu jambo ambalo linawezekana kutokana na kufanya vizuri kwa Arsenal dhidi ya City kwa siku za hivi karibuni.
Arsenal wamekuwa wababe kwa kushinda Michezo miwili Kati ya mitano dhidi ya Manchester city na Michezo iliyosalia wametoa sare.Wengi wanaamini rekodi hizo si kigezo cha kuibeza City ambayo imeamka kutoka usingizini na sajili za wachezaji kama Marc Guehi na Semenyo zimeleta mabadiliko katika maeneo ya ushambuliaji na ulinzi.
Washambuliaji wenye uwezo wa kipekee kama Omar Marmoush,Semenyo,Halaand wanategemewa kuibeba city dhidi ya Arsenal na kuuvunja mwiko uliodumu katika michezo 6 iliyopita.

0 Comments