Ligi ya Mabingwa Africa inaendelea jioni ya leo kwa raundi ya 5 ya makundi mbalimbali. Mashabiki wa soka Tanzania wamejiweka tayari kujua hatma ya timu zao pendwa za Simba na Yanga katika Michezo muhimu ya ugenini
HESABU ZA YANGA ZIMEKAA VIZURI
Klabu ya Yanga imesafiri mpaka nchini Morocco kuwakabili As far Rabbat. Huu ni mchezo mgumu zaidi kwa Yanga na wanapaswa kushinda au kutoa sare ili kujiweka katika mazingira mazuri ya kutinga robo fainali.Mchezo huu unapigwa saa nne usiku wa leo
Yanga wanashika nafasi ya 3 kwenye msimamo wa kundi B wakiwa na alama 5 Sawa na As far. Kama watashinda mchezo huo watafikisha alama 8 na kupanda mpaka nafasi ya 2 nyuma ya vinara Al Ahly wenye alama 8 mpaka sasa kabla ya mchezo dhidi ya Js Kablyie.
Kama Yanga watatoa sare dhidi ya As far basi watasalia nafasi ya 3 hivyo kujiweka katika nafasi nzuri katika mchezo wa mwisho dhidi ya Js Kablyie utakaopigwa dimba la nyumbani la Amaan Zanzibar.
Kama Yanga watapoteza mchezo huo kisha Js Kablyie wakiwa nyumbani kuwakabili Al Ahly na kushinda basi mambo yanaweza kuwa magumu zaidi kwa Yanga kwani timu hiyo itafikisha alama 5 Sawa na Yanga hivyo kundi hilo kuwa gumu zaidi kuelekea michezo ya mwisho.
KWA HESABU HIZI NI NGUMU SIMBA KWENDA ROBO FAINALI
Klabu ya Simba ipo Jijini Luanda nchini Angola kuwakabili Petro de Luanda. Matokeo ya Mchezo huu yataamua hatma ya Simba kuendelea au kuondoshwa kwenye mashindano.Mchezo huu utapigwa Saa moja usiku wa leo .
Simba wana alama Moja pekee katika Michezo 4 waliyocheza mpaka sasa na alama hiyo waliipata baada ya sare ya mabao 2-2 dhidi ya Esperance de Tunis.
Ushindi dhidi ya Petro de Luanda utaifanya Simba kufikisha alama 4 hapo wataomba dua ya ushindi kwa Stade mallien dhidi ya Esperance ambapo kinara Stade mallien atakuwa na alama 11 akifuatiwa na Esperance de Tunis alama 6 na Petro de Luanda alama 5.
Mchezo wa mwisho utakuwa dimba la Benjamin Mkapa na Simba atatakiwa kushinda dhidi ya Stade Mallien na kufikisha alama 7 kisha kukaa nafasi ya pili akiomba dua ya sare kati ya Esperance de Tunis akiwa ugenini dhidi ya Petro de Luanda na kama itakuwa hivyo timu Esperance watafikisha alama 7 Sawa na Simba huku Petro de Luanda wakifikisha alama 6 . Kama watatumia kigezo cha magoli mengi ya kufunga basi Simba wanaweza kwenda robo fainali ila kama wataangalia timu hizo zilipokutana basi Esperance de Tunis watakwenda fainali.



0 Comments