SIRI IMEFICHUKA NA WANAOIHUJUMU SIMBA WAJULIKANA

 Mara baada ya klabu ya Simba kutoa sare na Esperance de Tunis katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa uliopigwa dimba la Benjamin Mkapa na kuambulia alama 1 katika Michezo minne ya Kundi Shabiki na Mwanachama wake nguli Yericko ameandika waraka wa ushauri kwa Klabu hiyo.

"Kwaheri @simbasctanzania kwenye michuano ya Klabu Bingwa, Klabu bora imetolewa michuanoni.

Turudi mezani, tujisahihishe tumejivuruga sana, 

Ukweli unaanzia kwa Viongozi wa Simba wa pande zote, Wale wa @moodewji na wale wa Mangungu. Tatizo la simba liko hapo kwenye uongozi, sio wachezaji, tukipata tiba tutakuwa tumeitibu timu nzima. 

Mgogoro wa viongozi unahusu mchakato Mabadiliko ya uendeshaji wa klabu ambapo Upande wa Mo hautaki mabadiliko yanayopendekezwa na Serikali ambapo mabadiliko hayo yakipitishwa Mo ataondolewa nguvu zote katika klabu na anafikiri kwamba atakuwa hana udhibiti wa pesa zake anazowekeza, na Upande wa Mangungu hautaki mapendekezo ya upande wa Mo ambapo mapendekezo ya Mo yanampa nguvu ya moja kwa moja kuikamata timu na kuhakikisha udhitibi wa pesa yake anayowekeza. 

Mpasuko zaidi ulitokea katika mkutano mkuu wa mwaka huu pale Mwenyekiti wa Klabu Ndugu Mangungu alipowafanyia uhuni kwakuzuia maoni ya wanachama ambao walishagawanyika tangu msimu wa ligi ukiwa haujaanza kwa mabavu na ghiriba, Mangungu alipitisha rasmu ya mapendekezo yanayoungwa na serikali. 

Upande wa Moo ulipoona hivyo, sasa umeamua kukaa pembeni huku juhudi kubwa zikielekezwa kukwamisha mchakato na kukwamisha timu, Zingati timu yote 99.99% ni ya Mo, sasa waswalihili masikini wamelazimisha kile wanachoamini kitawapa nguvu ndani ya klabu lakini wamesahau kuwa hawana pesa na hawana shule ya mpira isipokuwa ni fitina ndogondogo na uchawi kiasi. Na hayo ndio matokei ya timu yetu…

Kwa msimu huu tusahau ubingwa wa ligi, hadi turejeshe ummoja ndani ya klabu hii, na ili kurejesha ummoja kuna mambo makuu mawili lazima yatendeke. 

1. Mangungu na genge lake waondoke klabuni, mchakato wa mabadilliko ya klabu urudi kwa wanachama turekebishe vipengele vinavyobishaniwa ndipo turudi serikali (BMT na RITA).

2. Moo aondolewe klabuni alipwe madeni yote anayotudai, achukue ile 20 yake aliyoweka kama dhamana, abaki kuwa mwanachama tu kisha tuendele na mchakato ule wa kihuni wa Mangungu na genge lake waliouoitisha bila wanachama kushirikishwa ambao sasa usubiri kuwasilishwa/umewasilishws serikalini kwa utekelezaji tu.

Na mechi ijayo Uto watatupiga kwa mara ya 7 mfululizo "

Post a Comment

0 Comments