UWANJA WA HOIMA WAGEUKA GUMZO KUELEKEA AFCON 2027

 Kuelekea Michuano ya AFCON 2027 inayoandaliwa na Kenya ,Uganda na Tanzania maandalizi yameendelea kushika kasi kwa nchi hizo hususani viwanja vitakavyotumika Kwenye michuano hiyo.

Leo tunaangazia uwanja wa Hoima city Stadium uliopo nchini Uganda.Uwanja huu umekamilika kwa asilimia 100 na unapatikana Jijini Hoima magharibi mwa Uganda.

Uwanja huu ulianza kujengwa August 2024 mpaka Novemba 2025 ukiligharimu taifa la Uganda kiasi cha dola milioni 131. Uwanja huo una uwezo wa kubeba watazamaji 20,000 waliokaa na ulijengwa na kampuni ya kituruki ya Summa international Construction Inc

Kwa mara ya Kwanza uwanja huo ulifunguliwa DISEMBA 24 ,2025 na uligeuka kivutio kwa waliohudhuria. Pembeni ya Uwanja huu kumejengwa Indoor Arena yenye kumbi za mikutano,kiwanja cha Basket Ball Chenye hadhi ya kimataifa na kiwanja cha mazoezi cha hadhi ya kimataifa. SBwawa la kuogelea lenye hadhi ya Olympic na viwanja vya Tennis vya kimataifa 

Uganda kama mmoja ya wenyeji wa Michuano ya AFCON 2027 itakuwa na viwanja vitatu vikubwa vitakavyotumika Kwenye michuano hiyo.

Kwa Upande wa Kenya na Tanzania ujenzi umeendelea kushika Kasi kwa viwanja vya Zanzibar Arena uliopo Zanzibar,uwanja wa Samia Suluhu uliopo Arusha na maboresho ya Uwanja wa Benjamin Mkapa uliopo Dar es salaam.

Uwanja mkubwa zaidi wa Raila Odinga uliopo Kenya unakaribia kukamilika na uwanja huo Una uwezo wa kubeba watazamaji 60,000 ukiwa na miundombinu ya kisasa.



Post a Comment

0 Comments