Utamu wa Michuano ya Ligi ya Mabingwa Africa na kombe la Shirikisho inazidi kupamba Moto na Tanzania yenye timu nne ikiendelea kwa kusuasua baada ya kucheza Michezo minne ya Awali
YANGA MAMBO YANAKWENDA VIZURI
Klabu ya Young Africans imeendelea kufanya vyema na kushika nafasi ya pili ikiwa na alama 5 kwenye msimamo wa kundi B nyuma ya Al Ahly wenye alama 8. Yanga inapaswa kushinda Michezo Yake miwili iliyobaki ili kujihakikishia nafasi ya kwenda robo fainali kwani As Far Rabbat na wao Wana alama 5 Sawa na Yanga lakini pia Wana mchezo wa marudiano na wababe hao wa Jangwani
AZAM FC WAMEREJEA KWA KISHINDO
Klabu ya Azam FC imepata ushindi katika mechi mbili dhidi ya Nairobi United na kufikisha alama 6 wakishika nafasi ya 3 kwenye msimamo wa kundi. Wanapaswa kushinda mechi zote mbili ili kujiweka kwenye nafasi ya kwenda robo fainali ya Shirikisho.
Wydad Casablanca na Maniema Union wanaongoza kundi hilo wakiwa na alama 9 kila mmoja na Azam atasafiri mpaka Morocco kuwakabili Wydad huku mchezo WA mwisho akimalizia Zanzibar dhidi ya Maniema Union.
SINGIDA NJIA YAKE NI NGUMU BILA HESABU
SINGIDA Black Stars wamepata alama 4 katika Michezo 4 na kushika nafasi ya 3 nyuma ya cr belouizdad wenye alama 9 na Otoho d'oyo wenye alama 6. Ili kuvuka kundi C SINGIDA anapaswa kushinda mechi zote na kufikisha alama 10 na Hilo linawezekana endapo Wakiweka juhudi katika mechi hizo mbili za Ugenini na Nyumbani
SIMBA WAKO TAABANI
Klabu ya Simba imepata alama 1 pekee katika Michezo 4 iliyocheza ikitoa sare 1 na kupoteza Michezo mitatu. Mchezo unaofuata watakwenda Angola kuwakabili Petro De Luanda na mchezo wa mwisho watawakaribisha Stade Mallien. Simba wanapaswa kushinda michezo hiyo ili kurudisha Imani kwa Mashabiki wake lakini kama watapoteza mchezo mmoja Kati ya miwili waliyonayo basi watatolewa mashindanoni




0 Comments