ARSENAL WAUKARIBIA UBINGWA WA EPL

 Klabu ya Arsenal imeendelea kuusogelea ubingwa wa EPL baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Everton. 



Katika mchezo huo mgumu uliopigwa dimba la Emirates uliishuhudia Arsenal ikipata bao la uongozi dakika ya 89 kupitia kwa Gyokeres na bao la pili likiwekwa kimiani na Dowman dakika ya 90+7.

Matokeo hayo yamewafanya Arsenal kufikisha alama 70 katika Michezo 31 na kusalia kileleni kwa tofauti ya alama 9 zaidi ya Manchester City wenye alama 61 katika Michezo 30.

Kwa sasa Arsenal wanahitaji alama 12 pekee ili kutangazwa mabingwa wapya wa EPL na kuvunja mwiko wa kutotwaa ubingwa huo kwa Miaka 20 tangu walipofanya hivyo mwaka 2006 chini ya Kocha Arsene Wenger 

Michezo iliyosalia kwa Arsenal 



Post a Comment

0 Comments