Katibu wa kamati ya mashindano wa kamisheni ya ngumi za kulipwa nchini Tanzania TPBRC, Ibrahim Kamwe amesemaa chama cha makocha wa ngumi za kulipwa Tanzania TPBCA, kimefanya maamuzi sahihi ya kumteua Dauka Somba kuwa afisa habari wao.
Kamwe ametoa kauli hiyo leo katika ofisi za TPBRC zilizopo jijini Dar es salaam huku akimpongeza Somba na kumkaribisha katika utendaji wa majukumu yake hayo mapya.
"Kwanza kabisa niwapongeze chama cha makocha kwa kukuteuwa wewe kama meneja wa habari na mawasiliano.
"Hilo ni jambo bora sana kutokana na mchango wako mkubwa unaouonesha katika mchezo wa ngumi wamelenga mtu husika kwahiyo nawapongeza sana chama cha makocha kwa kuliangalia hilo.
"Tunategemea mengi sana kutoka kwako sisi kamisheni tunahitaji vijana damu changa kama nyinyi kwaajili ya kuendeleza ngumi.
"Karibu sana pengine kwa wakati ujao tunaweza tukakuomba uwepo kwetu hapa (TPBRC) karibu sana na hongera sana kwa kupeleka mchezo wa ngumi hatua moja kwenye hatua nyingine," amesema Kamwe.

0 Comments