Dakika 90 na zile 30 za nyongeza za mchezo wa fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kati ya Arsenal na PSG zilikamilika huku timu zote mbili zikiwa sare ya 1-1. Mikwaju ya penati ikaamua mshindi PSG ikipata penati 4- 3.
Arsenal walitangulia kwa bao la mapema lililofungwa na Kai Havertz katika dakika ya 6, kabla ya PSG kusawazisha kupitia penalti ya Ousmane Dembélé katika dakika ya 65.
Mchezo huo ulikuwa na ushindani mkali, Arsenal wakionekana kuwa na nidhamu nzuri ya ulinzi huku PSG wakitawala zaidi umiliki wa mpira na kujaribu kutengeneza nafasi.
PSG inakuwa timu ya pili kuandika historia katika muongo uliopita kwa kuweza kutetea taji hilo, ililolitwaa msimu uliopita kwa kuchapa Inter Milan 5-0, ikifuata nyayo za Real Madrid
Vitinha awa gumzo
Nyota huyo mwenye miaka 26 alikokota mipira mara 162 na kupiga jumla ya pasi fupi 141 pasi ndefu 4, mashuti yaliyoelekea langoni 4 na kunyang'anya mipira mara 5.
Nyota huyo aliifanya Arsenal ishindwe kucheza vyema hasa eneo la katikati lililokuwa linaundwa na Declan Rice pamoja na Myles Lewis Skelly
LUIS ENRIQUE AFIKIA REKODI ZA GUARDIOLA,ZIDANE UEFA
Msimu wa 2024/25 alitwaa taji la pili akiifunga Inter Milan kwa mabao 5-0 na msimu huu ameifunga Arsenal kwa mikwaju ya penati 4-3
Kocha huyo amezifikia rekodi za Pep Guardiola aliyeisaidia Barcelona kutwaa taji la UEFA msimu wa 2009 na 2011 akiifunga Manchester United kisha kutwaa taji la tatu akiwa na Manchester City baada ya kuifunga Inter Milan bao 1-0.
Kocha Carlo Ancelotti anasalia kinara wa kom,be hilo akitwaa mara mara 5 akiwa na AC Milan vikombe viwili mwaka 2002/2003 na 2006/2007 .Real Madrid mwaka 2014,2022 na 2024

.webp)

0 Comments