MATAJIRI WAKOSHWA NA SIMBA QUEENS WAMWAGA MAMILIONI

 Klabu ya wanawake ya Simba Queens imefanikiwa kutwaa ubingwa wa ligi kuu ya wanawake msimu wa 2025/26 baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 5-2 dhidi ya Mashujaa fc. Ushindi huu umewafanya Simba Queens kufikisha alama 52 katika michezo 18 wakishinda michezo 17 na sare 1 wakitofautiana kwa alama 10 na Yanga Princes wenye alama 42 na timu zote kubakiwa na michezo 2.



Simba Queens chIni ya kocha Hassan Mgosi imekuwa na mwendelezo mzuri msimu huu wakifunga mabao 48 na kuruhusu mabao 7 pekee.Mara baada ya Mchezo dhidi ya Mashujaa kumalizika Mwekezaji na mdhamini wa Simba Bw.Mohammed Dewji ameandika ujumbe kwa wachezaji hao

''Hongereni Simba Queens kwa kutwaa ubingwa wa ligi kwa mara nyingine tena. Kwa mafanikio ya mataji matano ya ligi na kufika hatua ya nusu fainali ya CAF Women’s Champions League, Simba Queens imeendelea kujidhihirisha kama moja ya timu zilizoweka alama kubwa zaidi katika soka la wanawake nchini Tanzania.

Mafanikio haya yanatupa sababu ya kujivunia, lakini bado tuna malengo makubwa zaidi.Lengo letu ni kuona Simba Queens ikitwaa ubingwa wa CAF Women’s Champions League na kuipeperusha bendera ya Tanzania barani Afrika.Hongereni Simba Queens. Safari bado inaendelea''

Naye mlezi wa klabu hiyo Fatema Dewji aliwakabidhi wachezaji hao kiasi cha shilingi milioni 10 kama pongezi kwa uwezo mzuri waliouonyesha msimu huu na kunukuliwa akisema 

''Asante kwa kila mchezaji, benchi la ufundi, viongozi, mashabiki na wadau wote walioamini safari hii. Huu ni mwanzo wa mafanikio makubwa zaidi kwa Simba Queens…tukiwa mabingwa wa Tanzania, sasa macho yetu yanaelekezwa kwenye ushindani wa kimataifa na kuendelea kuipeperusha bendera ya Simba na Tanzania kwa ujumla

Post a Comment

0 Comments