Michuano ya Kombe la Dunia imeendelea kushika kasi nchini Marekani,Canada na Mexico na sasa tupo hatua ya Nusu fainali inayowakutanisha Ufaransa dhidi ya Hispania na Uingereza dhidi ya Argentina.
Tukiwa katika hatua hii Timu mbalimbali zimeweka rekodi zilizotikisa ulimwengu wa soka,Wachezaji wenye majina makubwa wameendelea kuwa gumzo kutokana na umahiri mkubwa waliouonyesha kwenye hatua za makundi,32 Bora,16 Bora na sasa Nusu fainali.Amospoti imekuletea mambo matano yaliyotikisa katika hatua hizo.
1. Mabao na pasi za Mwisho
Jumla ya Michezo 100 imeshachezwa mpaka sasa na katika Michezo hiyo jumla ya mabao 292 yamefungwa Sawa na wastani wa mabao 2.92 kwenye kila mchezo uliochezwa. Lionel Messi na Kylian Mbappe wanaongoza orodha ya ufungaji Bora wakifunga mabao 8 kila mmoja wakati Olise akiongoza orodha ya utoaji pasi za mabao akifanya hivyo mara tano. Timu ya taifa ya taifa ya Argentina inaongoza kwa kufunga mabao ikiwa na mabao 17 ikifuatiwa na Ufaransa yenye mabao 16.
Ufaransa inaongoza kwa pasi nyingi za Mwisho ikiwa imepiga pasi 14.Timu ya taifa ya Panama imemaliza mashindano hayo bila kufunga bao lolote.
2. Muitikio wa mashabiki
Jumla ya mashabiki milioni 6.25 wameingia viwanjani kushuhudia michuano hiyo Sawa na asilimia 99.7. Mchezo wa raundi ya 16 Kati ya Uingereza na Mexico uliweka rekodi ya kuwa mchezo ulioingiza mashabiki wengi zaidi na kutazamwa zaidi kupitia televisheni , mashabiki milioni 36 waliutazama mchezo huo.
Uwanja wa Mexico Stadium unashikilia rekodi ya kuingiza mashabiki wengi ,zaidi ya mashabiki 80,824 walihudhuria katika kila mechi iliyochezwa uwanjani hapo na kuufanya uwanja huo kuingiza jumla ya mashabiki 404,120 katika mechi 5 zilizochezwa.
3.Ushiriki wa kidijitali na mitandao ya kijamii
Kulikuwa na maonyesho (impressions) bilioni 30, mwingiliano wa watu bilioni 1.7 na mara bilioni 14.5 ambazo video zilitazamwa kwenye majukwaa yaliyopendelewa ya TikTok na YouTube, na hivyo kufikisha jumla ya mara bilioni 20 ambazo video zilitazamwa. Takwimu hizi zote ni za juu zaidi kuliko zile za Kombe la Dunia la FIFA la mwaka 2022 kwa idadi sawa ya siku za mashindano hayo. Maonyesho kwenye mitandao ya kijamii yameongezeka kwa asilimia 130, mwingiliano umeongezeka kwa asilimia 160 na idadi ya mara video zilitazamwa imeongezeka kwa asilimia 485.
Video ya sherehe ya 'Viking Row' ndiyo iliyotazamwa zaidi kwenye TikTok ikiwa na mara milioni 174, ikifuatiwa na ile ya Neymar akiwapongeza wachezaji wa Norway (milioni 70). Onyesho la Shakira na Burna Boy la wimbo wa 'Dai Dai' katika mechi ya ufunguzi limepata mara milioni 135 za kutazamwa kwenye Instagram na milioni 49 kwenye YouTube. Kwenye YouTube, bao la kwanza kabisa la Cristiano Ronaldo katika hatua ya mtoano ya Kombe la Dunia la FIFA lilifikisha mara milioni 75 za kutazamwa. Video inayoonyesha hisia za watu kuhusu bao la Luis Romo katika mechi kati ya Mexico na Jamhuri ya Korea, iliyorekodiwa kwenye Tamasha la Mashabiki wa FIFA jijini Mexico City, bado ndiyo video iliyotazamwa zaidi kwenye Facebook ikiwa na mara milioni 82.



0 Comments