WORLD CUP 2026:UJERUMANI YATUKUMBUSHA ILIVYOICHAKAZA BRAZIL

 Timu ya Taifa ya Ujerumani imeanza kwa kishindo michuano ya Kombe la Dunia 2026 baada ya kuichakaza CURACAO kwa mabao 7-1 mchezo wa kwanza Kundi E.

Felix Nmecha alikuwa wa kwanza kupachika bao la ufunguzi dakika ya 6 akimalizia pasi ya Florian Wirtz. Dakika ya 21 Comenencia aliisawazishia  Curacao bao hilo. Dakika ya 38 Ujerumani walipata bao la pili kupitia kwa Schlotterbeck akimalizia pasi ya Nathaniel Brown .Dakika ya 45 Kai Havert alipachika bao la tatu kwa mkwaju wa penati na mpira kwenda mapumziko Ujerumani wakiongoza kwa mabao 3-1.

Dakika ya 47 Musiala alipachika bao la nne Ujemani akipokea pasi kutoka kwa Joshua Kimmich.Nathaniel Brown aliipa Ujerumani bao la tano dakika ya 68 akimalizia pasi kutoka kwa Deniz Undav ambaye alipachika bao la sita akimalizia pasi kutoa kwa Joshua Kimmich.

Kai Havert alipachika bao la saba kwa ujerumani dakika ya 88 na kufikisha mabaio mawili katika mchezo huo uliokuwa na kasi.

Matokeo hayo yanaifanya Ujerumani kuongoza kundi E wakiwa na alama 3 na mabao 7 ya kufunga. Tangu kuanza mwaka 2002 Ujerumani imeendelea kushikilia rekodi ya kufunga mabao mengi zaidi katika mechi moja ikiifunga Hungary mabao 8-0 mwaka 2002 michuano iliyofanyika Korea Kusini na Japan. Mwaka 2014 iliifunga Brazil mabao 7-1 michuano iliyofanyika nchini Brazil na 2026 imeifunga Curacao mabao 7-1 michuano inayofanyika nchini Marekani,Canada na Mexico.

Mchezaji bora wa mechi

Kipindi cha kwanza Felix Nmecha alianza kwa kishindo baada ya kupachika bao la Uongozi dakika ya 6 kisha kuchezewa madhambi ndani ya 18 na refarii kuamuru mkwaju wa penati iliyopigwa na  Kai Harvet aliyefunga bao la tatu kwa Ujerumani.Matukio hayo muhimu yalimfanya Felix Nmecha kuwa mchezaji bora wa mchezo kwa kipindi cha kwanza.

Bao la pili lililofungwa na Kai Harvert lilibadili mitazamo ya wadau wa soka na hatimae tuzo ya mchezaji Bora wa mchezo ilikwenda kwa Harvert



Post a Comment

0 Comments