Taarifa kutoka kwa chanzo cha karibu na timu ya bondia Mtanzania Hassan Mwakinyo zinasema bondia huyo alihujumiwa siku mbili kabla ya pambano, chanzo kinasema hofu ya hujuma hiyo ni kuwa imefanywa kupitia chakula, maji ya kunywa ama mfumo wa hewa katika kambi yake.
Bondia Mwikinyo alijikuta dhaifu kupindukia licha ya mazoezi ya kuupa mwili nguvu na dua maalum kutoka kwa sheikh aliyesafiri nae, timu yake ilimshauri asitumie tena maji na chakula cha anapoishi badala yake watumie chakula kutoka nje ya eneo hilo.
“Bondia alikua dhaifu sana baada ya kufika katika kambi, kambi ambayo promota wa pambano alikua akikaa hapo pia, ilibidi utaratibu wa chakula ubadilishwe, bondia alianza kutumia maji ya chumvi ya bahari na visomo ndio vilimuweka sawa kidogo.”
“Hata hivyo timu haikuridhika na hali yake kabla ya pambano ikamshauri aghairishe pambano, lakini mwenyewe aligoma akihofia maneno ya kuonekana ameogopa, hivyo akaendelea na pambano na kutokea kilichotokea.”
Kinasema chanzo. .. Nani anakataa kama hujma hazipo michezoni ilhali timu zetu tu hapa kila siku zinakimbia vyumba vya kubadilishia nguo, nani anakataa kwamba hakuna hujuma michezo ilhali National Al Ahly na timu nyingine huwa zinakuja na vyombo vyao hapa kama mapima nk.
Mwakinyo pole ya kupoteza pambano katika mtindo wa kikatili, bado una dhamana ya kupeperusha bendera ya taifa hili la Tanzania, the hard way is the only way, no retreat no surrender bro, lets keep on pushing.
Ameandika mjomba wangu AMES ANDREW

0 Comments