WORLD CUP 2026: DAKIKA ZA JIONI JAPAN YAZIMA SHANGWE LA UHOLANZI

 Kombe la dunia linaloendelea nchini Marekani,Mexico na Canada limeendelea kuleta msisimko wa kipekee kutokana na ubora wa timu shiriki. Usiku wa jana tuliishuhudia  mechi yenye upinzani mkali ikizikutanisha Morroco kutoka Afrika dhidi ya Brazil ya America Kusini mchezo uliomalizika kwa sare ya 1-1. 

Leo usiku tumeishuhudia Ujerumani ikiweka rekodi ya kipekee kwa kushinda mabao 7-1 dhidi ya Cuacaro.Hayo yote tisa ,Mchezo wa kundi F uliozikutanisha Japan ya Asia dhidi ya Netherlands ya Ulaya umezua gumzo kutokana na umahili wa mchezo wenyewe.


SARE YA KIBABE 

Mchezo huo wa kasi na ufundi mwingi ulipigwa dimba la Dallas ambapo Netherlands walijipatia bao la uongozi dakika ya 51 kupitia kwa Virgil Van Djik . Dakika ya 57 Keito Nakamura aliisawazishia Japan lakini Crysencio Summerville wa Netherlands alipachika bao la pili dakika ya 64. 

Daichi Kamada aliwazima mashabiki wa Netherlands kwa kupachika bao la 2 dakika ya 89 na mchezo kumalizika kwa sare ya mabao 2-2. Matokeo hayo yanawafanya Netherlands na Japan kuongoza Kundi F wakiwa na alama 1 kila mmoja huku mchezo kati ya Sweden na Tunisia utaamua nani aongoze kundi F.

VAN DIJK NYOTA WA MCHEZO

Ubora wa Virgil Van Dijk haujawahi kushuka hasa katika mechi muhimu za kimashindano. Beki huyu wa Kati aliibeba Safi ya ulinzi ya Netherlands na kwa hakika amestahili kutwaa tuzo ya mchezaji Bora dhidi ya Japan.

Bao la dakika ya 51 pamoja na kuthibiti kwa ufasaha washambuliaji wa Japan kumemfanya nyota huyo kuibuka mchezaji Bora wa mechi hiyo ya kundi F na hiyo ndiyo tafsiri halisi ya Unahodha


Post a Comment

0 Comments