LAMINE YAMAL NA BAHATI YA KUKUTANA NA GOATS

Lamine Yamal anatajwa kama mchezaji  mrithi wa nafasi ya Lionel Messi na Cristiano Ronaldo. Nyota huyu raia wa Hispania amepata bahati ya kipekee msimu huu wa Kombe la Dunia 2026 kwa kukutana na Cristiano Ronaldo katika hatua za robo fainali na kushinda mchezo huo kwa bao 1-0. 

Nyota huyo akiwa na wenzake walifanikiwa kuiondosha Ufaransa katika hatua za Nusu fainali yenye Mshindi wa Ballon d'Or 2025 Ousman Dembele na Mfungaji Bora wa muda wote wa Kombe la Dunia Kylian Mbappe.  

Lamine Yamal na Lionel Messi watakutana katika fainali za Kombe la Dunia itakayopigwa tarehe 19 Julai. Lamine Yamal anatajwa kama mchezaji bora chipukizi wa mashindano hayo akiwa na mabao matatu na kufanikiwa kutwaa tuzo ya mchezaji Bora wa mechi mara 3. Lionel Messi anawania tuzo mbili mpaka sasa. Messi Anatajwa kama mchezaji Bora wa mashindano kwa kutwaa tuzo sita za mchezaji bora pamoja na kuwania kiatu cha Mfungaji Bora akiwa na mabao 8 nyuma ya  Kylian Mbappe mwenye mabao 10.

Msimu Bora kwa Lamine Yamal 

Nyota huyu wa Barcelona amekuwa gumzo tangu alipojiunga na Miamba hiyo ya Hispania. Lamine ni zao la La Masia na tangu alipopandishwa kikosi cha Kwanza amekuwa Moto wa kuotea mbali. Msimu wa 2025/26 Lamine aliiongoza Barcelona kutwaa ubingwa wa La Liga akifunga mabao 16 na kutoa pasi za mabao 12. Nyota huyo pamoja na Ferran Torres  walitwaa tuzo ya Zara wadhamini wa Barcelona. Nyota huyo aliiongoza Barcelona kutwaa ubingwa wa Super Copa Espana kwa kuibamiza Real Madrid kwa mabao 3-2 na ametwaa tuzo ya mchezaji Bora wa msimu. 

Je Lamine Yamal  ni Pele au Lionel Messi Mpya?

Hayati Edson Arantes do Nascimento maarufu kama Pele anatambulika kama mfalme wa football baada ya kutwaa kombe la Dunia mara tatu kuanzia mwaka 1958,1962 na 1970. Pele alipata umaarufu akiwa na miaka 17 baada ya kufunga mabao mawili dhidi ya Sweden na kuisaidia Brazil kutwaa ubingwa wa Dunia. Nyota huyo ndiye mchezaji Bora wa Karne ya 20. Kama  Lamine Yamal atatwaa ubingwa wa Dunia basi tutamtambulisha kama mwana wa mfalme Pele. Ingawa Lamine Yamal ana miaka 19 lakini sote tumeushuhudia uwezo wake kuanzia Timu ya Taifa alipoisaidia kutwaa ubingwa wa Euro 2024 mbele ya Uingereza yenye nyota mahili kama Rashford,Harry Kane, Declan Rice na Pickford. Ubingwa huu wa Dunia utampeleka kwenye viwango vingine .

Kama Lamine tutamwita Messi Mpya basi atakuwa na kazi kubwa mno ikiwamo kutwaa tuzo 7 za Ballon d'or,kuvunja rekodi nzito na kutwaa mataji mengi zaidi .

Itaendelea........










Post a Comment

0 Comments