Kylian Mbappé ametangazwa kuwa mchezaji atakayeonekana kwenye jalada la mchezo wa video wa EA Sports FC 27.Mshambuliaji huyo wa Ufaransa na Real Madrid amewahi kuonekana kwenye jalada la mchezo wa awali wa soka wa EA Sports, FIFA, katika miaka ya 2021, 2022 na 2023.
Mbappé ataonekana kwenye jalada la matoleo yote mawili, la kawaida na lile la 'Ultimate', la mchezo wa EA Sports FC 27.
Hivi karibuni alishinda tuzo ya 'Golden Boot' katika Kombe la Dunia, akifunga mabao 10 katika michuano hiyo ambayo pia ilimfanya ampiku Lionel Messi kama mfungaji bora katika historia ya mashindano hayo.
"Kuonekana kwenye jalada la mchezo wa EA Sports FC kwa mara ya kwanza ni tukio la kipekee sana kwangu," alisema Mbappé.
"Ni heshima kuendeleza uhusiano wangu wa muda mrefu na mfululizo huu wa michezo katika awamu yake mpya, nikiwa pamoja na wachezaji ambao wameunda historia yake.Nasubiri kwa hamu kila mtu aupate uzoefu wa mchezo wa FC 27."
Video ya kuonyesha jinsi mchezo huo unavyochezwa inatarajiwa kutolewa na EA Sports siku ya Alhamisi.Mchezo wenyewe kamili unatarajiwa kuzinduliwa mwezi Septemba.


0 Comments