TETESI ZA USAJILI DUNIANI 23.7.2026

 Liverpool wana imani kuwa wanaweza kuwashinda Arsenal na Bayern Munich katika mbio za kumsajili mshambuliaji wa Paris Saint-Germain, Bradley Barcola, baada ya kuchangia mabao manne katika Kombe la Dunia akiwa na Ufaransa. (The Sun)


Arsenal wanaonekana kuwa mbele katika mbio za kumsajili kiungo wa Bournemouth, Alex Scott (miaka 22), ambaye pia anawindwa na Manchester United. Hata hivyo, Scott ana wasiwasi kuhusu kupata muda wa kutosha wa kucheza katika Uwanja wa Emirates. (Daily Mirror)

Scott pia anapendelea kuhamia Chelsea, baada ya Bournemouth kukataa ofa ya pauni milioni 64 kutoka kwa Blues. (The Standard)

End of Unaweza kusoma

Alex Scott

Chanzo cha picha,Getty Images

Kiungo wa Manchester United, Bruno Fernandes (miaka 31), ameamua kuendelea kubaki klabuni, huku mazungumzo ya kuongeza mkataba mpya yakiendelea. (Daily Express)

Besiktas wanajaribu kumsajili kiungo wa Newcastle United, Joe Willock (miaka 26), ambaye amebakiza mwaka mmoja kwenye mkataba wake na hatapewa mkataba mpya. (The Telegraph)

Arsenal hawajafunga mlango wa kumuuza nahodha wao Martin odegaard (miaka 27), na wako tayari kusikiliza ofa kwa kiungo huyo wa Norway. (TeamTalk)

Martin odegaard

Chanzo cha picha,Getty Images

Manchester United wanafikiria kufanya uhamisho wa kiungo wa Real Madrid, Eduardo Camavinga (miaka 23), ambaye alikosa nafasi katika kikosi cha Ufaransa cha Kombe la Dunia msimu huu wa joto. (Nicolo Schira)

Post a Comment

0 Comments