SIMBA YAJA KIVINGINE DHIDI YA COASTAL UNION

 Klabu ya Simba imetangaza rasmi mabadiliko ya uwanja wake wa nyumbani kutoka KMC kwenda Meja Isamuyo. Hayo yamewekwa wazi na afisa habari wa klabu hiyo Ahmed Ally kuelekea mchezo wa raundi ya tatu wa Ligi kuu ya NBC dhidi ya COASTAL UNION 

Ahmed Ally amenukuliwa akisema "“Taarifa ya kwanza iwafikie Wanasimba inahusu mwendelezo wa Ligi Kuu ya NBC tunapenda kutangaza kwamba mechi zetu za nyumbani tutatumia Uwanja wa Meja Isamuhyo, awali tulitangaza tutatumia Uwanja wa Uhuru lakini sasa tunatangaza tutatumia Uwanja wa Meja Isamuhyo. uwanja ambao tulitumia vyema msimu uliopita, ni ngome yetu ya ushindi na kwa mantiki hiyo turejee tena katika uwanja huo. Nitumie nafasi hii kuwashukuru wamiliki wa uwanja, JKT kwa kuturuhusu na sisi kuwa wenyeji wa uwanja huo. Tutaanza kutumia uwanja huo kwenye mchezo dhidi ya Wagosi wa Kaya, mchezo ambao utapigwa Agosti 27, 2026.”

“Kumekuwa na changamoto ya maendeleo ya mfumo mpya wa ununuaji wa tiketi ambao sasa tiketi inanunuliwa kupitia simu ya mkononi. Kwa mashabiki wa Simba hasa wa nyumbani hili kwao linakuwa geni. Mechi yetu ya Agosti 27, 2926 ndio itakuwa mechi ya kwanza mashabiki wengi kukutana na mfumo huu, ni mfumo rahisi kununua tiketi lakini sababu ni mfumo mpya. Ni mfumo rahisi sababu huitaji kwenda kituoni kununua tiketi, ulipo hapohapo kupitia simu unaweza kununua tiketi, dunia imeshahama kwenye kupanga foleni kununua tiketi.”

“Viingilio katika mchezo dhidi ya Coastal itakuwa ni Tsh. 5,000 kwa Mzunguko na Tsh. 10,000 kwa VIP A. Tunafahamu uwanja uko mbali kidogo lakini haina budi kwa Wanasimba kupokea uwanja huo. Msimu uliopita ambao tulicheza kwenye Uwanja wa Meja Isamuhyo hatukupoteza mchezo hata mmoja, ni sehemu salama kwelikweli kwa upande wetu.”

“Kikosi kilirejea jana kutoka Singida na leo kikosi kimeanza mazoezi kujiandaa na mchezo dhidi ya Coastal Union.”- Semaji Ahmed Ally. #NguvuMoja

Post a Comment

0 Comments